Michuano ya Tennis kwa Vijana wenye umri chini ya
miaka 16 ukanda wa Afrika Mashariki inaanza hapo kesho jijini Dar es
Salaam Tanzania ikishirikisha timu 8.
Timu zinazotaraji kushiriki ni wenyeji Tanzania,
Rwanda,Burundi,Kenya,Seychelles, Comoro, Ethiopia, na Sudan. Makamu wa
Rais wa Shirikisho la Tennis Tanzania,Bi Fina Mango ambaye pia ni
Mkurugenzi wa mashindano hayo amesema kuwa Michuano ya Mwaka huu mbali
na kuongezeka idadi ya Timu zinazoshiriki yaani timu 8,lakini pia timu
zitakazoshika nafasi tatu za juu zitafuzu kushiriki michuano ya Afrika
ya mchezo huo inayotaraji kufanyika nchini Kenya baadae mwezi March
mwaka huu.
Naye Mwakilishi wa Shirikisho la Kimataifa la
Mchezo huo ITF Bwana Thierry Ntwali kutoka Burundi amesema juhudi
zimekuwa zikifanyika kuinua mchezo wa Tennis katika ukanda wa Afrika
Mashariki ambapo amesema hivi sasa nchini Burundi kumeanzishwa Kituo cha
Kimataifa cha kuwaendeleza Vijana chipukizi wanaoonyesha Kipaji katika
Mchezo huo,huku Michuano ya Mwaka huu inayoanza hapo kesho ikitaraji
kuibua Vipaji vipya.
Kwa upande wake Kocha msaidizi wa Timu ya Tennis
ya Tanzania Nicholas Jonas amesema wachezaji wake wamejiandaa Vema
kutwaa Ubingwa wa Michuano hiyo ambayo mwaka Uliopita Timu ya Tanzania
ilishika nafasi ya Pili na kwa kuwa wachezaji wengi ni wale wale
waliocheza mwaka uliopita basi mwaka huu ni nafasi yao ya kutwa Ubingwa
wa Michuano hiyo inayotaraji kuanza kesho tarehe 12 hadi tarehe 19 mwezi
huu wa January 2014.
No comments:
Post a Comment