KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Monday, January 6, 2014

Onyo latolewa, afya ya Schumacher

Meneja wa bingwa mara saba wa mashindano ya magari ya langalanga ya F1, Michael Schumacher, ameonya dhidi ya taarifa za upotoshaji zinazotolewa na baadhi ya watu kuhusu afya ya mwanamichezo huyo. Onyo hili limekuja baada ya mtu mmoja kukaririwa akisema maisha ya Schumacher hayako hatarini.
Schumacher bado yuko katika hali "mahututi japo imara" katika hospitali huko Grenoble nchini Ufaransa baada ya ajali ya kuanguka na kupigiza kichwa kwenye mwamba wakati akiteleza katika theluji ya milima ya Alps.
Taarifa kutoka kwa meneja Sabine Kehm imesema taarifa zote ambazo hazitolewi na mameneja au madaktari, lazima zichukuliwe kama "uzushi mtupu".
Taarifa hiyo pia imekanusha ripoti ya kutokabidhiwa kwa hiyari, Camera iliyokuwa imefungwa katika kofia ngumu "helmet" ya Schumacher wakati wa kuteleza, kuwa hazina ukweli.

No comments:

Post a Comment