UCHAGUZI Mkuu wa Chama
cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), utafanyika Februari
16 mwaka huu jijini Dar es Salaam. Uamuzi huo ulifikiwa na kikao cha
Kamati ya Utendaji ya TASWA kilichofanyika Dar es Salaam jana kujadili
masuala mbalimbali ya chama na waandishi wa habari za michezo kwa
ujumla.
Kikao kilikubaliana kuwa uchaguzi ufanyike kwa katiba ya zamani,
kwani mchakato wa katiba mpya unaweza kuchukua muda mrefu, hivyo
kusababisha viongozi waliopo madarakani kuendelea kukalia viti kinyume
cha katiba, jambo ambalo si sahihi.
Kutokana na hali hiyo viongozi wapya
watakaochaguliwa moja ya kazi yao kubwa itakuwa kuifanyia marekebisho
makubwa katiba ya chama chetu ili iende na wakati. Fomu za kuwania
uongozi zitaanza kutolewa Februari 10 hadi Februari 14 mwaka huu saa
kumi alasiri, masuala mengine yahusiyo uchaguzi huo, ikiwemo mahali
utakapofanyika yatatangazwa baada ya kikao cha sekretarieti ya TASWA na
Kamati ya Uchaguzi kitakachofanyika Februari 3.
No comments:
Post a Comment