'Under-fire' David Moyes wa mashetani wekundu ameteuliwa kwenye kinyanganyiro cha meneja bora wa Premier League wa mwezi Disemba.
Mskochi huyo amepoteza michezo yote mitatu ya michuano ya mbalimbali tangu mwaka huu kuanza lakini akiwa na kumbukumbu ya ushindi wa michezo minne na sare moja katika mwezi wa mwisho wa kumalizia mwaka 2013.
Bosi wa Chelsea Jose Mourinho pia ameteuliwa baada ya kuongoza kikosi chake kwa ushindi mara tano katika michezo saba, akipata sare moja ugenini dhidi ya Arsenal na kupoteza mchezo mmoja.
Manuel Pellegrini pia ameteuliwa baada ya kuiongoza Manchester City na kushinda michezo sita na sare moja katika jumla ya michezo saba ya mwezi huo na pia wakiendelea kukamua idadi kubwa ya mabao.
Wa mwisho ni bosi wa Everton Roberto Martinez, ambaye alishuhudia kikosi chake kikipata ushindi michezo minne katika jumla ya michezo sita, huku wakipoteza mchezo nyumbani dhidi ya Sunderland likiwa ni doa pekee katika rekodi yao katika uwanja wa nyumbani kwa mwaka 2013.

Luis Suarez anaongoza orodha ya wafumania nyavu bora wa mwezi, akifuatiwa na Yaya Toure, Vincent Kompany, Alvaro Negredo, Ross Barkley na Theo Walcott.
No comments:
Post a Comment