KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Thursday, February 13, 2014

Kombe la shirikisho:Leverkusen chali, Dortmund, Munich, Kaiserslautern na Wolfsburg wapeta nusu fainali

Mchezaji wa Bayer Leverkusen Sydney Sam akiugulia maumivu
Katika kinyang'anyiro cha kombe la shirikisho , DFB Pokal, timu nne zimefanikiwa kuingia duru ya nusu fainali. Timu hizo ni Borussia Dortmund, Bayern Munich, Kaiserslautern na Wolfsburg. 

Jana timu ya daraja la pili ya Kaiserslautern iliiondoa Bayer Leverkusen katika kinyang'anyiro cha kombe la shirikisho la Ujerumani DFB Pokal katika mchezo wa robo fainali, baada ya kushinda kwa bao 1-0 katika mchezo ambao ulichezwa kwa muda wa dakika 120 baada ya timu hizo kutoka sare bila kufungana katika muda wa kawaida.
DFB-Pokal Viertelfinale Bayer 04 Leverkusen 1. FC Kaiserslautern Wachezaji wa Kaiserslautern wakishangiria ushindi

Wolfsburg iliishinda nguvu Hoffenheim kwa mabao 3-2 na Bayern Munich ilidhihirisha ubabe wake kwa kuishinda Hamburg kwa mabao 5-0.
Timu nne Wolfsburg, Kaiserslautern, na Bayern Munich zimeingia nusu fainali ambapo Borussia Dortmund ilikuwa timu ya kwanza kukata tikiti yake kwa kuishinda Eintracht Frankfurt kwa bao 1-0 siku ya Jumanne.

No comments:

Post a Comment