MECHI TANO VPL KUCHEZWA JUMAMOSI
Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara inaingia raundi ya 19 kesho (Februari 22 mwaka huu) kwa mechi tano zitakazochezwa katika miji ya Dar es Salaam, Bukoba, Morogoro, Tanga na Arusha.
Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara inaingia raundi ya 19 kesho (Februari 22 mwaka huu) kwa mechi tano zitakazochezwa katika miji ya Dar es Salaam, Bukoba, Morogoro, Tanga na Arusha.
Yanga itakuwa mgeni wa Ruvu Shooting ya mkoani Pwani katika mechi
itakayofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Nayo Kagera Sugar
inaikaribisha Rhino Rangers ya Tabora katika mchezo utakaofanyika Uwanja
wa Kaitaba mjini Bukoba.
Uwanja wa Manungu uliopo Turiani mkoani Morogoro ndiyo utakaotumika
kwa mechi kati ya Mtibwa Sugar na Ashanti United, wakati Coastal Union
itaumana na Mbeya City katika mechi itakayooneshwa moja kwa moja na Azam
Tv kutoka Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.
Maafande wa Oljoro JKT watakuwa nyumbani kupambana na Mgambo Shooting
katika mchezo utakaofanyika kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh
Kaluta Amri Abeid jijini Arusha.
Jumapili (Februari 23 mwaka huu) katika Uwanja wa Taifa ni Simba
dhidi ya JKT Ruvu, mechi ambayo pia itaoneshwa moja kwa moja na Azam Tv.
Mechi kati ya Azam na Tanzania Prisons iliyokuwa ichezwe kesho
(Februari 22 mwaka huu) Uwanja wa Chamazi sasa itachezwa Jumapili
(Februari 23 mwaka huu) ambapo na itakuwa ‘live’.
Ligi hiyo itaendelea Jumatano (Februari 26 mwaka huu) kwa mechi moja
kati ya Ashanti United na Azam itakayochezwa kwenye Uwanja wa Azam
Complex (Chamazi).
TWIGA STARS, ZAMBIA SASA KUCHEZA FEB 28
Mechi ya pili ya raundi ya kwanza kuwania Kombe la Afrika kwa
Wanawake (AWC) kati ya Tanzania (Twiga Stars) na Zambia (Shepolopolo)
sasa itachezwa Februari 28 mwaka huu Uwanja wa Azam Complex uliopo
Chamazi, Dar es Salaam.
Twiga Stars tayari ipo kambini kujiandaa kwa mechi hiyo itakayochezwa
kuanzia saa 10 kamili jioni. Twiga Stars chini ya Kocha Rogasian
Kaijage inafanya mazoezi yake kwenye Uwanja wa Karume ambao ni wa nyasi
za bandia kama ulivyo ule wa Azam Complex.
Shepolopolo iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 katika mechi ya kwanza
iliyochezwa Februari 14 mwaka huu kwenye Uwanja wa Nkoloma jijini
Lusaka.
Iwapo Twiga Stars itafanikiwa kuiondoa Shepolopolo itacheza na
mshindi wa mechi kati ya Botswana na Zimbabwe. Zimbabwe ilishinda mechi
ya kwanza ugenini.
Wachezaji wa Twiga Stars waliopo kambini ni Amina Ali, Anastazia
Katunzi, Asha Rashid, Donisia Minja, Esther Chabruma, Etoe Mlenzi,
Everine Sekikubo, Fatuma Issa, Fatuma Makusanya, Fatuma Mustafa, Fatuma
Mwisendi, Fatuma Omari, Flora Kayanda, Happiness Mwaipaja, Maimuna
Mkane, Mwajuma Abdallah, Mwapewa Mtumwa, Pulkeria Charaji, Sherida
Boniface, Sophia Mwasikili, Therese Yona, Vumilia Maarifa na Zena Said.
MICHUANO YA MIKOA KUSAKA VIPAJI YATIMUA VUMBI
Michuano ya mikoa katika mpango maalumu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kuboresha Taifa Stars inaanza kutimua vumbi kesho (Februari 22 mwaka huu) kwa mechi nne.
Michuano ya mikoa katika mpango maalumu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kuboresha Taifa Stars inaanza kutimua vumbi kesho (Februari 22 mwaka huu) kwa mechi nne.
Mechi rasmi ya ufunguzi wa michuano hiyo inayodhaminiwa na
Kilimanjaro Premium Lager itakuwa kati ya Ilala na Temeke. Mechi hiyo ya
kundi G itachezwa Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume kuanzia saa 9.30
alasiri.
Kundi A kutakuwa na mechi kati ya Pwani na Morogoro kwenye Uwanja wa
Mabatini mjini Mlandizi wakati Kusini Unguja na Kaskazini Unguja
zitacheza kwenye Uwanja wa Mao Tse Tung mjini Unguja katika kundi H.
Kusini Pemba na Kaskazini Pemba zitacheza mechi ya Kundi I katika Uwanja wa Gombani kisiwani Pemba.
Mechi za keshokutwa (Februari 23 mwaka huu) ni Simiyu itacheza na
Shinyanga mjini Bariadi katika kundi E. Nayo Ruvuma itacheza na Njombe
kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea katika kundi D.
Kundi C ni Tanga na Kilimanjaro kwenye Uwanja wa Mkwakwani wakati
Kagera itacheza na Geita kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba katika
kundi B. Mtwara itacheza na Lindi kwenye Uwanja wa Nangwanda mjini
Mtwara katika kundi F.
Wang’amuzi 40 wa vipaji tayari wamesharipoti kwenye vituo vya mechi hizo kwa ajili ya kufanya kazi hiyo.
No comments:
Post a Comment