Bingwa Mtetezi wa mbio za New York Marathon Geoffrey 
Mutai alitoka nyuma na kuthibitisha udedea wake katika barabara za mji 
huo wa Marekani alipokata utepe akitumia muda wa saa moja na sekunde 
hamsini.
                     
Muingereza Mo Farah, hata hivyo, ndiye 
aliyewaduwaza mashabiki wake nchini Marekani alipokunguwaa na kuanguka 
baada ya takriban kilomita tisa na kisha akajifua na kurejea kwa 
kishindombio zikikaribia kukamilika .
                     
Bingwa huyo wa mbio za mita elfu 
tano na mita elfu kumi za olimpiki alimaliza katika nafasi ya pili 
sekunde 18 pekee nyuma ya Mkenya mshikilizi wa muda bora katika mbio za 
marathon duniani.
                     
Farah alishikwa na kisunzi punde baada ya kukamilisha mbio hizo na alilazimika kubebwa kwa machela.
                     
Mo Farah azirahi baada ya kukamilisha mbio za New York
Muingereza huyo baadaye alisema alikuwa sawa na 
kuwa ataendelea na mazoezi yake kabla ya kushiriki mbio zake za kwanza 
za marathon katika mashindano ya London Marathon zitakazoandaliwa mwezi 
ujao.
                     
Mkenya mwengine Stephen Sambu alimaliza katika nafasi ya tatu sekunde moja pekee nyuma ya Mo .
                     
Ilikuwa siku njema kwa wakenya kwani Sally 
Kipyego vilevile kutoka Kenya alitwaa ubingwa wa kitengo cha wanawake 
akisajili muda wa saa moja dakika 8 na sekunde 31.
                     
Muda huo ndio wa kasi zaidi katika kitengo hicho cha wanawake.
                     
Bizunesh Deba, kutoka Ethiopia alimaliza wapili huku Mmarekani Molly Huddle akikamilisha orodha ya tatu bora.
                     
Wanariadha 20,000 walistahimili kiwango cha nyuzijoto zaidi ya 30 na kushiriki mbio hizo za kilometer 21 .

No comments:
Post a Comment