Kiungo Athumani Iddi
‘Chuji’ amebaki Dar es Salaam huku kiungo mshambuliaji wa timu hiyo, Emmanuel
Okwi akiwa bado kwenye mgomo.
Yanga ipo Arusha kwa ajili ya mechi hiyo ya Ligi Kuu Bara ambapo
ushindi ni muhimu kwao ili iendelee kuwania kutetea taji lake ambalo pia
linaweza kutua Azam ikiwa watashinda mechi ya kesho dhidi ya Mbeya City.
Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara timu ya Young
Africans kesho watashuka dimbani kusaka pointi 3 muhimu kwa kucheza na
timu ya JKT Oljoro mchezo utakaofanyika kwenye dimba la Uwanja wa Sheikh
Amri Abeid jijini Arusha.
Kikosi cha Young Africans kiliwasili jana jioni jijini Arusha na
kufikia katika hotel ya Joshmal eneo la stand na leo asubuhi wachezaji
wamefanya mazoezi kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid ambao ndio
utakaotumika kwa mechi kesho.
Kocha
Mkuu wa Young Africans Hans van der Puijm amesema anashukuru vijana
wake wako salama, wachezaji wote 23 waliopo kambini jijini Arusha wako
fit kwa kuajili ya kusaka pointi 3 muhimu ambazo zitaisogeza kwene
nafasi nzuri ya kutetea Ubingwa.
Young Africans inashika
nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom ikiwa na pointi 52
nyuma ya Azam FC yenye pointi 55 huku timu zote zikiwa zimebakisha
michezo miwili kabla ya kumalizika kwa ligi.
Wachezaji waliopo kambini jijini Arusha ni:
Walinda milango: Deogratias Munish "Dida" na Ally Mustafa "Barthez"
Walinzi: Juma Abdul, Mbuyu Twite, Oscar Joshua, Amos Abel, Rajab Zahir, Ibrahim Job, Kelvin Yondani na Nadir Haroub "Cannavaro".
Viungo: Hamis Thabit, Nizar Khalfani, Frank Domayo, Hassan Dilunga, Salum Telela na Sospter Maiga
Washambuliaji: Didier Kavumbagu, Hamis Kizza, Jerson Tegete, Mrisho Ngasa, Saimon Msuva, Said Bahanuzi na Hussein Javu
No comments:
Post a Comment