KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Saturday, May 17, 2014

Southampton yaacha wachezaji kibao wakiwemo Guly do Prado, Lee Barnard na Forte

Southampton imewaachilia wachezaji Guly do Prado, Lee Barnard na Jonathan Forte baada ya kumaliza mikataba yao.
Mbrazil Do Prado mwenye umri wa miaka 32, alifunga magoli 23 baada ya kuicheza klabu hiyo jumla ya michezo 118 katika kipindi cha misimu minne ndani ya klabu hiyo. 

Mshambuliaji huyo aliisaidia klabu hiyo kushinda katika kampeni za kupanda daraja na kutinga Premier League, lakini ameichezea michezo 12 tu katika kikosi cha kwanza msimu huu. 

Barnard mwenye umri wa miaka 29, alielekea kwa mkopo katika klabu ya Southend United wakati ambapo Forte mwenye umri wa miaka 27, alikopeshwa Sheffield United katika msimu wa 2012-13. 

Cody Cropper, Lloyd Isgrove, Sam McQueen, Omar Rowe na Jake Sinclair wamepewa ofa ya kuongeza mikataba yao ili kuendelea kusalia ndani ya klabu hiyo baada ya ushiriki wao mkubwa katika kikosi cha kwanza msimu wa 2013-14. 

Kuna wachezaji kadhaa vijana ambao wameachwa na klabu hiyo wakiwemo wachezaji walio katika mpango wa kuendeleza vipaji wakiwemo wachezaji  Matt Young, Joe Curtis na Andy Robinson.

Jamal Branker, Fraser Colmer, Charlie Higgins na James White pia wanaondoka katika klabu hiyo huku Tom Leggett na Isaac Nehemie wakijiunga na Aston Villa .

No comments:

Post a Comment