KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Saturday, May 3, 2014

Steven Gerrard kuendelea kusalia Anfield kwa mwaka mwingine

Brendan Rodgers ameliambia gazeti la Liverpool Echo kuwa ataangalia juu ya uwezekano wa kumuongezea mkongwe na nahodha wa klabu hiyo Steven Gerrard mkataba mpya wakati wa kiangazi.

Mkataba wa sasa wa Gerrard ndani ya Anfield utamalizika mwishoni mwa msimu ujao ambapo Rodgers tayari ameanza kufikiria kuongea muda kwa kiungo huyo.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 33 anafanya kazi kubwa na ngumu ya kuwaweka katika kilele cha msimamo wa ligi huku meneja huyo akiamini kuwa bado Gerrard ana mengi ya kuchangia ndani ya kikosi chake.

Akinukuliwa Rodgers amesema 
"Steven ni mmoja wa wale tunao waangalia kuwapa mkataba wakati wa kiangazi, licha ya kuwa na mwaka mmoja mbele"
"Naamini Steven atakuwepo 2015. Ni mchezaji ambaye ameonyesha ubora wake msimu huu"

No comments:

Post a Comment