KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Wednesday, July 23, 2014

Aishi Manula awaambia ukweli watanzania na kasumba zao za hovyo

Kipa Aishi Manula wa Azam fc na Taifa stars
Mlinda mlango namba mbili wa kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' Aishi Manula, amewataka watanzania kuwa na mtazamo chanya katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye mchezo wa pili wa kuwania kufuzu kucheza fainali za Afrika dhidi ya Msumbiji.

Aishi Manula ambaye ni mlinda mlango namba mbili nyuma ya Deodratius Munishi'Dida' amesema kuna haja kwa watanzania kuendelea kuiunga mkono Taifa Stars na kuacha kasumba ya kuwahukumu wachezaji kwa kigezo cha matokeo ya sare yaliyopatiakana.
Mlinda mlango huyo wa klabu ya Azam amesema mpaka sasa si Tanzania wala Msumbiji aliyejihakikishia nafasi ya kusonga mbele, hivyo umoja na mshikamano uliokuwepo kabla ya mchezo wa mwishoni mwa juma lililopita una mantiki kwa watanzania kuelekea kwenye mpambano wa mwanzoni mwa mwezi ujao.