KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Thursday, July 10, 2014

KOCHA LUIZ FELIPE SCOLARI NDO BASI TENA KUINOA BRAZIL VIONGOZI WAPYA WA CBF WAMTOSA

Big Phil Luiz Felipe Scolari ndio basi tena
Matarajio ya kocha mkuu wa timu ya taifa ya Brazil Luiz Felipe Scolari, ya kuendelea kukinoa kikosi cha timu ya taifa ya nchi hiyo yamaenza kuingia shakani, baada ya viongozi watakao liongoza shirikisho soka CBF kuanzia mwaka 2015 kuthibitisha hawatokuwa na mpango nae.
Viongozi watarajiwa na chama cha soka nchini Brazil, wametangaza mpango huo kufuatia Scolari kushindwa kutangaza kujiuzulu kutokana na kadhia ya kupachikwa mabao saba kwa moja, iliyomkuta siku mbili zilizopita huko Bero Horizonte mbele ya timu ya taifa ya Ujerumani.
Makamu wa rais wa chama cha soka nchini Brazil, Delfim Peixoto ambaye atashika hatamu ya uongozi wake kuanzia mwezi April mwaka 2015, amesema haoni sababu ya kocha huyo mwenye umri wa miaka 65, kuendelea kuwepo madarakani kutokana na tabia yake ya kufanya maamuzi binafsi pasina kusikiliza ushauri wa mtu mwingine.
Peixoto, amekiambia kituo cha televishani cha ESPN Brazil, kwamba Scolari alikuwa na kila sababu ya kuikwepa aibu iliyowakuta ya kuchabangwa mabao saba kwa moja, lakini mapungufu yake ndiyo chanzo cha hayo yote, hivyo anaona muda wa kustahafu kwa kocha huyo umewadia.
Wakati huo huo Luis Philipe Scolari amebadili kauli yake ya kutotarajia kujiuzulu na kusema huenda akatangaza mustakabali wa nafasi yake ndani ya kikosi cha timu ya taifa ya Brazil mara baada ya fainali za kombe la dunia.