KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Thursday, July 10, 2014

Kocha wa Argentina Alejandro Sabella, ametangaza kulipa kisasi dhidi ya timu ya taifa ya Ujerumani kwenye fainali

Kocha wa timu ya taifa ya Argentina Alejandro Sabella katikati akifurahia ushindi wa penati dhidi ya Uholanzi katika mchezo wa nusu fainali ya kombe la dunia nchini Brazil uliopigwa jana
Siku moja baada ya kujihakikishia nafasi ya kucheza hatua ya fainali, kocha wa timu ya taifa ya Argentina Alejandro Sabella, ametangaza kulipa kisasi dhidi ya timu ya taifa ya Ujerumani kwa niaba ya mataifa ya Amerika ya kusini yaliyoshiriki michuano ya kombe la dunia ya mwaka huu, huko nchini Brazil.

Sabella, ametangaza hali hiyo huku akitambua fika mashabiki wa soka wa ukanda wa Amerika ya kusini, watakua wanaiunga mkono timu yake ambayo itakua na shughuli ya kupambana na taifa kutoka barani Ulaya (Ujerumani).

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 59 amesema kikosi chake kipo tayari kupambana hadi tone la mwisho la jasho, kwa ajili ya kuhakikisha ubingwa unabaki kwenye ardhi ya bara la Amerika ya kusini.

Hata hivyo amesema mpango alioutangaza haumaanishi kama anawabeza wapinzani wao Ujerumani, bali anawaheshimu kutokana na mchezo mzuri wa soka walio uonyesha tangu alipoanza mshike mshike wa kushiriki fainali za kombe la dunia za mwaka huu.

Kauli ya Alejandro Sabella, huenda ikawapa faraja mashabiki wa soka wa nchini Brazil ambao bado wanakumbuka kichapo cha kadhia cha kufungwa mabao saba kwa moja kilichowaangukia siku mbili zilizopita kutoka kwa Ujerumani.

Mchezo wa kumsaka bingwa wa fainali za mwaka 2014, utachezwa siku ya jumapili katika uwanja wa Maracana uliopo mjini Rio de Janeiro, ukitanguliwa na mchezo wa kumsaka mshindi wa tatu utakaochezwa siku ya jumamosi kwenye uwanja wa Nacional Mané Garrincha, mjini Brasília kati ya wenyeji Brazil dhidi ya Uholanzi.