Mashabiki wa soka wa mkoa wa Tanga kesho watakuwa na burudani ya aina yake pale vilabu vya vikubwa Coastal Union na African Sports vitakapo uumana kutoa burudani ya Idi |
TIMU
za Coastal Union (Wagosi wa Kaya) na African Sports (Wanakimanumanu) zote kutoka mkoani Tanga kesho kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani watatoa burudani ya kumalizika mwezi mtukufu wa Ramadhani ikiwa ni siku ya idi pili.
Taarifa ya msemaji wa Coastal Union kwa mtandao wa Rockersports, Oscar Assenga imesema maandalizi ya
kuelekea mchezo huo yamekamilika kwa
asilimia kubwa na kinachosubiriwa na mechi hiyo itakayoanza saa kumi jioni
kwenye uwanja huo.
Akiongea na mtandao huu kocha wa Coastal Union Yusufu Chipo amesema baada ya kumaliza mechi hiyo timu hiyo itaelekeza mipango yake ya
kucheza mechi za kirafiki nyengine ili kuweza kujiweka imara kwa ajili ya
maandalizi ya msimu mpya wa ligi kuu soka Tanzania bara.
Amesema
wachezaji wa timu hiyo wataingia kwenye mechi hiyo kwa malengo ya kupata
ushindi ili kuweza kuendeleza rekodi ya kuwafunga wanakumanumanu hao ambao
msimu ujao watashiriki michuano ya ligi daraja la kwanza.
Kwa
upande wake afisa Habari wa African Sports Said
Karsandas amesema kuwa wamepania kushinda kwenye mechi hiyo ili kuweza
kurudisha ile heshima ya timu hiyo kwa wagosi hao wa kaya.
Kumbuka African Sports ambayo iliwahi kuwa tishio katika soka la Tanzania miaka ya mwishoni ya 1980' hivi sasa inapambana kurejea ligi kuu ya Soka Tanzania bara na inajiandaa na ligi daraja la kwanza ambayo inatarajia kuanza mapema mwezi wa Septemba.
No comments:
Post a Comment