Nahodha wa timu ya taifa ya Ghana,
Asamoah Gyan, amekanusha madai kuwa alimtoa kafara yake ambaye pia
alikuwa mwanamuziki mashuhuri nchini Ghana Castro.
Gyan amesema tetesi hizo ni za kushangaza sana wala hazina msingi.
Mwanamuziki
huyo aliyekuwa anaiimba nyimbo za mtindo wa Afrobeats, ambaye jina lake
halisi ni Theophilus Tagoe, alitoweka pamoja na rafiki yake Janet
Bandu, mnamo mwezi Julai.
Wawili hao walitoweka wakati walipokuwa
wamekwenda likizo na Gyan ambaye alikuwa mchezaji wa zamani wa
Sunderland, katika mji wa Ada.
Madai katika vyombo vya habari
nchini Ghana yanasema kuwa kutoweka kwa rafiki ya Gyan kumezua wasiwasi
baadhi wakidai kuwa huenda alimtoa kafara mwanamuziki huyo.
Castro na rafiki yake Bandu, walionekana kwa mara ya mwisho wakielekea baharini na baadaye iliarifiwa kuwa walizama.
Miili
ya wawili hao haikuwahi kupatikana na madai yaliendelea kusambazwa
mwezi huu wakati ambapo kakake Gyan, Baffour Gyan alidaiwa kuwa mmoja wa
genge la vijana waliowashambulia wandishi wa habari waliohoji maswali
kuhusu madai hayo.
Hata hivyo baadaye aliachiliwa na polisi waliokuwa wamemkata kwa lengo la kumfungulia mashitaka.
Tetesi hizo zilimfanya Gyan kuitisha mkutano na wandishi wa habari kuzungumzia madai hayo.
Wakili
wake Kissi Agbyabeng alitoa taarifa akisema kuwa familia ya Gyan
imeshangazwa sana na madai hayo na iliamua kutosema chochote ili polisi
waendelee na uchunguzi wao.
Taarifa hiyo ilisema: " Tumekuwa kimya
huku madai na tetesi zikienezwa kila upande katika vyombo vya habari.
Tumekuwa kimya sio eti kwa sababu tunaficha ukweli, bali kwa sababu
hatuoni umuhimu wa kusema kilichojiri mjini Ada. Tumekuwa kimya kwa
sababu tunataka polisi wafanye kazi yao bila kuingiliwa.''
No comments:
Post a Comment