KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Wednesday, September 24, 2014

Arsenal, Chelsea na Manchester City vitani kumuwania mlinda mlango mwenye umri wa miaka 15

Mlinda mlango Mile Svilar (katikati) anatakiwa na Arsenal, Chelsea na Manchester United
Arsenal, Chelsea na Manchester United wanaonekana kuingia katika vita ya kutaka kumsajili mlinda mlango Mile Svilar, mwenye umri wa miaka 15 ambaye anaonekana ni kama Thibaut Courtois anayeinukia.
Svilar, ambaye kwasasa yumo katika kitabu cha klabu ya Anderlecht ya nchini Belgium,anawavutia vilabu vya Premier League kufuatia kuonyesha uwezo mkubwa katika michuano ya vijana.
Tayari amesha fanya majaribio katika klabu ya Chelsea na akiwa amealikwa na Arsenal, huku United pia ikonyesha kumuhitajia mlinda mlango huyo kijana

Svilar, 15, is tipped to become the next Thibaut Courtois, the talented Chelsea and Belgium stopper
Svilar, mwenye umri wa miaka 15, anafananishwa na Thibaut Courtois

Lakini baba yake, ambaye ni mlinda mlango wa zamani wa klabu ya Antwerp Ratko Svilar, anasema hatakwenda popote kwa wakati huu.
Akiongea na Nieuwsblad amesema:
'Amefanya majaribio Chelsea na Manchester United wanamtaka. Kila mtu anamtaka.
'Lakini tayari tunamakubaliano na Anderlecht, ingawa hataweza kusajili mkataba mpaka atakapo fikisha miaka 16.