Maxime, alisema Jaja na Coutinho watapata tabu sana watakapokuwa wakicheza kwenye viwanja vya mikoani kutokana na kuwa vibovu
Baada ya kuiongoza timu yake kupata ushindi mnono wa mabao 2-0 dhidi ya Yanga katika mchezo wa ufunguzi wa ligi kuu ya soka Tanzania Bara.
Katika mchezo huo mshambuliaji Geilson Santos ‘Jaja’ alikuwemo katika kikosi cha Yanga ambapo kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar, Mecky Maxime, amewaponda Wabrazili hao wa Yanga akisema ni wachezaji wa Uwanja wa Taifa tu.
Mtibwa iliendeleza ubabe wake kwa Yanga kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro, Jumamosi iliyopita katika mchezo uliofanyika katika uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro huku mabao wa Mtibwa yakiwekwa kambani na mkongwe Mussa Hassani Mgosi na Ame Ali.
Baada ya mchezo huo, Maxime ambaye alimfunga kocha wake wa zamani wa Taifa Stars, Marcio, Maxime, alisema Jaja na Coutinho watapata tabu sana watakapokuwa wakicheza kwenye viwanja vya mikoani kutokana na kuwa vibovu.
Alisema katika mechi yao, Jaja alipata wakati mgumu sana kucheza kutokana na uwanja kuwa mbovu lakini kama angekuwa akicheza kwenye Uwanja wa Taifa, pengine angefanya maajabu kama ilivyokuwa dhidi ya Azam katika mchezo wa Ngao ya Jamii. Jaja alikosa penalti ambayo ingeweza kuipatia Yanga bao la kusawazisha.
“Jaja siyo mbaya ni mchezaji mzuri sana ila viwanja vya Tanzania vitamsumbua sana, mpaka aje kukaa sawa itamchukua muda mrefu.
“Kwa jinsi ninavyoona mchezaji huyo na mwezake watakuwa wakifanya vizuri tu watakapokuwa kwenye Uwanja wa Taifa kwa sababu ni mzuri ukilinganisha na hivi vya mikoani, ambavyo wachezaji wetu wamevizoea,” alisema Maxime.