KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Monday, October 6, 2014

JUMA LUIZIO KUWASILI KESHO KUANZA KAMBI YA STARS KWA AJILI YA MCHEZO DHIDI YA BENIN

Juma Luizi wa Zesco United kuwasili kesho kambini Stars
Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager imeingia kambini leo (Oktoba 6 mwaka huu) kwenye hoteli ya Accomondia jijini Dar es Salaam tayari kwa mechi dhidi ya Benin.

Timu hiyo chini ya Kocha Mart Nooij kesho (Oktoba 7 mwaka huu), Jumatano (Oktoba 8 mwaka huu) na Ijumaa (Oktoba 10 mwaka huu) saa 10 jioni itafanya mazoezi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mshambuliaji Thomas Ulimwengu kutoka timu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (RDC) na kiungo Mwinyi Kazimoto kutoka timu ya Al Markhiya ya Qatar tayari wametua nchini kujiunga na kikosi cha Taifa Stars.

Naye mshambuliaji Juma Liuzio kutoka timu ya Zesco ya Zambia anawasili nchini kesho (Oktoba 7 mwaka huu) mchana kwa ndege ya Kenya Airways akitokea Ndola kupitia Nairobi.
ajili ya mechi hiyo itakayochezwa kuanzia saa 11 jioni.

Kwa mujibu wa Kocha Nooij, timu hiyo itakuwa na vipindi (sessions) 11 vya mazoezi kabla ya kucheza na Benin (Squirrels). Stars itafanya mazoezi asubuhi na jioni kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa ambapo baadhi yatafanyika Uwanja wa Taifa, na mengine kwenye uwanja mwingine.

Wachezaji Thomas Ulimwengu na Mbwana Samata wanaochezea timu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) pamoja na Mwinyi Kazimoto anayechezea timu ya Al Markhiya ya Qatar wanawasili nchini kesho (Oktoba 6 mwaka huu).

Naye mshambuliaji Juma Liuzio anayechezea timu ya Zesco ya Zambia atawasili nchini keshokutwa (Oktoba 7 mwaka huu) kwa ndege ya Kenya Airways akitokea Ndola.