TFF kuendesha mashindano ya vijana chini ya miaka 12 |
Mashindano ya
Taifa kwa vijana wenye umri chini ya miaka 12 yatafanyika Desemba mwaka huu
jijini Mwanza.
Akizungumza
wakati wa kutangaza mpango wa programu ya vijana inayolenga Fainali za Afrika
za U17 mwaka 2019 ambapo Tanzania imeomba kuwa mwenyeji, Rais wa TFF, Jamal
Malinzi alisema mashindano hayo yatashirikisha kombaini za mikoa yote.
Mashindano
hayo yatafanyika kuanzia Desemba 6 hadi 12 Mmwaka huu, na timu zinatakiwa
kuwasili jijini Mwanza, Desemba 5 mwaka huu. Bajeti ya mashindano hayo ni sh.
milioni 350.
Rais Malinzi
aliwashukuru wakurugenzi wa shule za Alliance (James Bwire) na Lord Baden
Powell (Kanali mstaafu Idd Kipingu) kwa kukubali shule zao kuwa za kwanza
kuanzia programu hiyo ya vijana.
Pia
aliishukuru kampuni ya Symbion ambayo imetoa sh. milioni 100 kwa ajili ya
kuunga mkono mashindano hayo ya U12. Symbion ni moja ya wadau wanaoshirikiana
na TFF katika mpango wa miaka mitano ya programu za vijana.
Mkurugenzi wa
Symbion, Stewart John Hall aliwasilisha kwa waandishi wa habari programu hiyo.
No comments:
Post a Comment