KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Sunday, October 5, 2014

Yanga yatakata uwanja wa taifa dhidi ya JKT Ruvu, lakini bao la Jabir Aziz Stima funika bovu

Wachezaji wa Yanga wakiongozwa na Haruna Niyonzima aliyefunga goli la pili wakionyesha staili mpya ya ushangiliaji baada ya Niyonzima kuiandikia timu yake bao la pili
Yanga ya Dar es Salaam hii leo imeibuka na ushindi wa bao 2-1 dhidi ya timu ngumu ya JKT Ruvu katika moja ya michezo ya ligi kuu ya soka Tanzania bara mchezo uliofanyika uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.
Mabao ya Yanga alipatikana kupitia kwa mlinzi wa kati Kelvin Yondani aliyepokea mpira wa mwisho kutoka kwa kiungo Haruna Niyonzima baada ya mpira mrefu uliopigwa na Gerson Santos Jaja.
Bao la pili lilifungwa na Haruna Niyonzima aliyepiga mpira wa adhabu uliokwenda moja kwa moja wavuni na kumuacha mlinda mlango wa JKT Ruvu Jackson Chove akishindwa hata kutikisika.
Hata hivyo ikiwa imesalia dakika mbili mpira kumalizika kiundo wa zamani wa Azam fc Jabir Aziz Stima aliiandikia JKT Ruvu bao la kufutia machozi akiwa umbali wa yadi zaidi ya 25 kutoka lango la Yanga.
Mlinzi wa kati wa Yanga Kelvin Yondani akipongezwa na wachezaji wenzanke baada ya kuiandikia timu yake bao la kwanza
Bao hilo lilionekana kumkuna hata kocha Yanga Mbrazil Marcio Maximo ambaye baada ya mchezo kumalizika alimwita kiungo huyo na kumkumbati kuonyesha ishara ya kukubali goli hilo.

No comments:

Post a Comment