KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Sunday, November 2, 2014

Mourinho ana matumaini kuwa Costa atarejea katika kiwango muda si mrefu

 Jose Mourinho ana matumaini kuwa Diego Costa ni hipi punde tu atarejea katika kiwango chake baada ya kurejea uwanjani kufuatia kuwa katika kaumivu na kucheza katika mchezo wa ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya QPR.

Costa alikosekana katika michezo minne ya Chelsea iliyopita muda kufuatia maumivu aliyorejea nayo akitokea katika majukumu ya kimataifa.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 26 alirejea katika kikosi cha kwanza mchezo dhidi ya kikosi cha Harry Redknapp uwanja wa Stamford Bridge, lakini alionekana kuwa hoi katika kipindi cha kwanza kabla ya kubadilishwa katika dakika ya 78.

Meneja wake Mourinho amesema anaamini kuwa Costa atarejea sawasawa katika kiwango chake kilicho mzalishia mabao nane katika msimu wake wa kwanza katika ligi kuu ya England.

No comments:

Post a Comment