KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Sunday, November 2, 2014

Mvua kubwa iliyonyesha jijini Tanga yapelekea mchezo wa Mgambo JKT na Mbeya City kuahirishwa

Mchezo wa ligi kuu ya soka Tanzania bara baina ya wenyeji Mgambo JKT ya Tanga dhidi ya Mbeya City ya Mbeya umeshindwa kufanyika kufuatia mvua kubwa iliyonyesha jijini Tanga hii leo.

Mchezo huo uliokuwa usimamiwe na mwamuzi Izrael Mujinu Nkongo sasa utafanyika kwa mujibu wa kanuni hapo kesho endapo hali ya hewa itakuwa imetulia jijini humo.

Kwa mujibu wa msimamizi wa mchezo huo mwamuzi mstaafu Hamisi Kisiwa mara baada ya ukaguzi kufanywa na waamuzi wa mchezo huo iliamuriwa mchezo huo kusogezwa mbele kwa saa 24 kwa mujibu wa kanuni huku taarifa zaidi ikisubiriwa kutoka kwa wasimamizi wa ligi hiyo bodi ya ligi.

No comments:

Post a Comment