KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Wednesday, August 25, 2010


Liverpool inataka EURO milioni €30 kwa ajli ya kumtoa Javier Mascherano baada ya kugomea mpango wa kubadilishana na Aliaksandr Hleb
Liverpool imewaaleza Barcelona ya kwamba inahitaji pauni milioni £24.5 ambazo ni sawa na EURO milioni €30 cash kwa ajili ya kumuuza kiungo wao Javier Mascherano na kukataa mpango uliopendekezwa na Barcelona wa kubadilishana na nyota wao Aliaksandr Hleb .
Licha ya taarifa kuchomoza huku nyuma ya kuwa Barca imeweka mezani pauni milioni £12m ,mabingwa hao wa Primera Division kiukweli ni kwamba sasa wameweka offer ya pauni milioni £18.8 wakimjumuisha na nyota wa Aliaksandr Hleb ili kumpata muajentina Mascherano mwenye umri wa miaka 26.
Hata hivyo Liverpool wanasema hawako tayari kwa mpango huo wa mchezaji ukijumlisha na pesa na wanacho taka wao ni cash.
Barcelona wanataraji kurejea tena ndani ya saa 48 kukamilisha mpango mzima huku tayari kukiwa na taarifa kuwa mwenyewe mascherano amekubaliana na Barca juu ya kile kinachoitwa “personal terms” na kigogo hicho cha Catalan.
taarifa toka ndani ya klabu zinasema klabu hiyo ilikuwa na mpango wa kumuuza mwezi januari na kwamba huenda thamani yake ingepungua baada ya kusalia Anfield.
Katika michezo miwili ya hivi karibuni ya ufunguzi wa ligi Mascherano alikuwepo dimbani ikiwa ni pamoja na mchezo wa sare ya bao 1-1 dhidi ya Arsenal.
Jana alimwambia kocha Roy Hodgson alikuwa hajisikii kucheza dhidi ya Manchester City katika mchezo ambao walimbwela kwa kichapo cha mabao 3-0 katika dimba la City of Manchester.
Katika hatua nyingne kocha wa Barcelona Pep Guardiola amesema anakila sababu ya kuongeza kiungo mkabaji katika timu yake lakini ameshindwa kuthibitisha juu ya ujio Javier Mascherano na wala kuonyesha kama ndiye mchezaji target no 1.
Alipoulizwa kama mabingwa hao wa Hispania wako kwenye mpango wa kumnasa nyota huyo Guardiola amsema .
"nitamzunguzia mara baada ya mchezaji huyo kuwasili lakini akamtaka muuliza swali alielekeze swali lake kwa sporting director Andoni Zubizarreta.


Mlinzi wa Algeria Halliche akamilisha usajili na kujiunga na Fulham
Fulham imethibitisha kumsajili mlinzi wa Algeria Rafik Halliche kwa mkataba wa miaka mitatu akitokea katika ya Benfica ya Ureno.
Halliche mwenye umri wa 23 ameelekea Craven Cottage kwa ada ambayo haijawekwa wazi baada ya kumvutia kocha Mark Hughes wa Fulham.
Akikaririwa Halliche anasema
"ninafuraha juu ya kukamilika kwa uhamisho wangu kuelekea Fulham ".
"kwangu Premier ndiyo “best league” duniani ambapo ninaweza kucheza na wachezaji wazuri na kupata fursa ya kushindana na timu zilizo bora kwahiyo kuwepo katika timu kama Fulham ni kitu ambacho kilikuwa kama ndoto.''
Halliche alijiunga na Benfica mwaka 2008 lakini kwa kipindi cha misimu miwili alikuwepo kwa mkopo katika klabu ya Nacional, na huu unakuwa ni usajili wa tatu kwa kocha Hughes baada ya Philippe Senderos, Jonathan Greening na Moussa Dembele.

No comments:

Post a Comment