KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Wednesday, August 25, 2010

SIMBA NA YANGA WAGOMEA MAPATO YA MCHEZO WAO WA NGAO YA HISANI NA MAKATO YA MAMLAKA YA MAPATO
Vilabu vya Simba na Yanga kwa pamoja vimekubaliana kutochukua mapato yaliyopatikana katika mchezo wao wa ngao ya jamii hadi pale shirikisho la soka nchini TFF pamoja na mamlaka ya mapato nchini TRA watakapoacha kukata mapato kwa vilabu.
Hatua hiyo imekuja kufuatia kikao cha pamoja kati ya vilabu hivyo kilichokutana hapo jana na kujadili mambo mbalimbali yaliyojitokea katika mchezo huo hususani suala zima la mgawanyiko wa mapato.
Wakizungumza na wanahabari maafisa habari wa vilabu hivyo kwa upande wa Simba Cliford Ndimbo na kwa upande wa Yanga Luis Sendeu wamesema kufuatia kikao hicho wamekubaliana kwa pamoja kutochukua mapato hayo kutokana na kutoridhishwa na ukatwaji wa mapato unaofanywa na TFF.Vilabu hivyo vimepewa shilingi milioni 33 kila kimoja baada ya mchezo ulioingiza milioni 222

No comments:

Post a Comment