KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Friday, August 13, 2010

MANCHESTER CITY NEWS
Man City sign Balotelli, Milner to follow

Hatimaye Manchester City imekamilisha zoezi la kunasa saini ya mshambuliaji wa Italia Mario Balotelli akitokea Inter Milan kwa ada ya uhamisho iliyoripotiwa kuwa ni pauni za kingereza milioni 24.

Balotelli mwenye umri wa miaka 20 amefanikisha vipimo vya afya alivyofanyiwa huku Manchester ijumaa ya tarehe 13 na kusaini mkataba wa miaka mitano na sasa akikamilisha uhamisho wake kutoka katika ligi kuu ya Italia “Serie A” na kuelekea katika ligi ngumu ya Uingereza “Premier League”.

Meneja wake mpya wa City Roberto Mancini ambaye aliwahi kufanya naye kazi huko nyuma katika klabu ya Inter Milan kabla ya kuelekea Eastlands amekaririwa akisema maneno haya kwa kimombo
"I think that Mario is one of the best players of his age in Europe.
"His style of play will suit the Premier League, and because he is still so young there is a big chance for him to improve. He is a strong and exciting player, and City fans will enjoy watching him.''
Licha ya mpango huo umekamilika ukiwa umechelewa kwa Balotelli kuwepo katika kikosi cha mchezo wa ufunguzi wa ligi dhidi ya Tottenham Hotspur kule White Hart Lane nyota huyo atakosekana katika mchezo huo lakini atakuwepo dimbani katika mchezo dhidi ya Liverpool August 23.
Mancini sasa anajipanga kumnasa James Milner akitokea Aston Villa

No comments:

Post a Comment