KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Tuesday, August 17, 2010

SIMBA VS YANGA
Kuelekea kwenye mchezo wa kesho wa ngao ya hisani mchezo ambao utawakuwanisha mahasimu wakubwa wa soka nchini Tanzania Simba na Yanga,Wekundu wa msimbazi almaarufu kama Mnyama ametua jiji Dar es Salaam hii leo wakitokea visiwani Zanzibar walipokuwa wameweka kambi maalum kwa ajili ya mchezo huo lakini pia kwa ajili ya ligi kuu ya kandanda Tanzania bara
Mnyama Simba kesho atakuwa akikutana na mabingwa wa zamani wa ligi kuu ya Tanzania bara Dar es Salaam watoto wa Jangwani Dar Young Africans katika mchezo ambao utakuwa ukipigwa katika uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.
Yanga yenyewe itakuwa ikitokea mkoni pwani bwagamoyo ambako walikuwa huko kwa takribani juma moja na siku kadhaa wakiwa huko kwa maandalizi ya mchezo huo wa kukata na mundu.
Mchezo wa kesho utakuwa una sura tofauti tofauti ikiwa ni pamoja na vikosi vyote kuwa na wachezaji wapya kadhaa ambao wamesajiliwa ndani ya msimu huu huku pia wakiwa nchini ya uongozi mpya .
Simba watakuwa wakiingia dimbani chini ya uongozi wa mwenyekiti Ismail Aden Rage ilhali Yanga kwa upande wao wakiwa chini ya mwenyekiti mpya Loyd Nchunga
KWA Upande wa mabenchi ya ufundi vikosi vyote vitakuwa chini ya makocha waliowahi kukutana katika msimu uliopita simba chini ya mzambia patrick phiri aliyerejea nchini hivi karibuni baada ya kutikisa kibiriti na kutikisa mtaa wa msimbazi vilivyo huku kwa upande wake wao Yanga wakiwa chini ya Costadin Papic maarufu kama “Clinton”
KUBWA katika mchezo wa kesho ni kikosi gani kilicho imara kabla ya kuanza kwa ligi kuu ya kandanda Tanzania bara baina ya vilabu hivyo viwili.
Wekundu wa Msimbazi Simba ambao walikuwa wamejificha visiwani Zanziabar kwa ajili ya maandalizi ya mchezo huo wamewasili majira ya saa sita mchana na boti la Kilimanjaro na kushuhudiwa na meza ya michezo na burudani .


KIKOSI KIPYA CHA SIMBA SPORTS CLUB

KIKOSI KIPYA CHA DAR ES SALAAM YOUNG AFRICANS

No comments:

Post a Comment