![]() |
Mashabiki wa timu ya taifa ya Ujerumani |
Mashabiki wa
soka nchini Ujerumani walioko katika michuano ya Euro wamekiponza chama chao
cha soka kufuatia kupigwa faini ya Euro 25,000 na shirikisho la soka barani
Ulaya UEFA kutokana na vurugu za mashabiki wake.
Mashabiki wa
Ujerumani wametuhumiwa kwa kitendo cha kuonyesha mabango yaliyokuwa yakiuunga
mkono neo-Nazi katika mchezo wa
hatua ya makundi dhidi ya Denmark ikiwa na pamoja kuwasha moto na kuimba nyimbo
za kibaguzi.
UEFA imeikabili
DFB na kuwapiga faini hapo jana baada ya kubaini kuwa vitendo vya mashabiki hao
ni kinyume cha maadili ya kisoka.
Taarifa ya
UEFA inasomeka
"chama
cha soka cha Ujerumani (DFB) kimepigwa faini ya euro 25,000 na bodi ya
kudhibiti vitendo vya kinidhamu ya UEFA ".
No comments:
Post a Comment