![]() |
Olivier Giroud |
The Gunners wamethibitisha
rasmi kupitia mtandao wa klabu hiyo kuwa imekamilisha makubaliano ya kumsajili
Mfaransa Olivier Giroud mkataba wa muda mrefu akitokea Montpellier bila kuweka
wazi dau lake.
Arsenal
ilikuwa ikihusishwa na mfaransa huyo muda mrefu ambapo sasa wameamua
kuhangaikia taratibu za uhamisho na tayari amefanikiwa kipimo cha afya yake
alicho fanya hapo jana.
Giroud amekuwa
na Montpellier katika ligi ya Ufaransa Ligue 1 na kutwaa taji msimu wa 2011-12.
Amefunga jumla ya mabao 21 katika jumla ya michezo 36 na meneja wa Arsenal Arsene
Wenger sasa anamsubiri Emirates Stadium kwa mkataba wa muda mrefu.
Giroud anaungana
sasa na wafaransa wenzake Laurent
Koscielny, Bacary Sagna, Sebastien Squillaci, Abou Diaby na Francis Coquelin mjini
London.
No comments:
Post a Comment