![]() |
Mesut Ozil |
Mesut Ozil anasema
kuelekea katika mchezo wa nusu fainali Euro 2012 dhidi ya Italia wako sawa na
watafanikiwa kutinga hatua ya fainali.
Italy imefanikiwa
kutinga nusu fainali baada ya kuwachapa Waingereza kwa njia ya penati katika
mchezo wa robio fainali uliopigwa jumapili iliyopita lakini kwasasa wanapimwa
mbele ya Ujerumani wakionekana si lolote si chochote.
Licha ya
Ujerumani kutokuwa na rikodi nzuri ya kuifunga Italia katika mashindano makubwa
, Ozil anaamini kiu yao hiyo itafikia mwisho kule Warsaw siku ya alhamisi na
kucheza fainali na ama Hispania au Ureno.
Ananukuliwa akisema
"mambo
ya nyuma si kitu ,"anasema Ozil .
Ameongeza
"timu nyingine zinatuheshimu lengo letu
ni kurejesha taji la Ulaya nchini Ujerumani tuko hapa kwa ajili hiyo. Tunaweza kuwafunga
Italia.
No comments:
Post a Comment