Cole na Young
wote walikosa penati katika mchezo wa jumapili wa robo fainali dhidi ya Italia
na simba watatu kutolewa
mashindanoni huku wachezaji hao wakianza kutupiana matusi kupitia mtandao wa kijamii wa
Twitter
Taarifa ya
FA imesema
"tunaingilia
kati moja kwa moja taarifa zinazohusu kutuwa matusi wachezaji hawa wawili wa
timu ya taifa ya Uingereza Ashley Cole na Ashley Young kupitia Twitter,''.
"wamejitolea
kila kitu kwa timu yao ya taifa katika Euro 2012 inatisha na haikubaliki jumbe
za aina hiyo ya matusi kutumwa.
Tunaunga
mkono uchunguzi wa polisi ili kubaini nani anachochea hili.''
Msemaji wa
polisi “Metropolitan Police Service” amenukuliwa akisema
"tunafuatilia juu ya maoni ya kibaguzi
kupitia Twitter katika mchezo wa usiku wa jana na tumeanza uchunguzi.
"uchunguzi
ulianza kufanywa na MPS jana na mjumbe mmoja wa uchunguzi wa kufuatilia maoni
kupitia mtandao wa kijamii wa twitter hususani maoni yanayotoka jijini London.
Hakuna mtu
mpaka sasa aliyewekwa kizuizini kuhusiana na hilo. MPS inaangalia uwezekanao wa
kufungua mashtaka kupitia kifungua 18/19
Public Order Act 1986.''
Watumiaji wa
Twitter waliendelea kutoa maoni yao kuwakosoa Young na Cole lakini baadae ikaandikwa
"ninachoweza kusema yote hayo ni
utani jamani achaneni na hili, police wanajua nilikuwa natania na nina
matumaini hawatanisumbua, cheers.''
Mwanafunzi mmjoa
toka Wales Liam Stacey aliwahi kwenda
jela kwa siku 56 mapema mwaka huu kwa kumdhihaki kibaguzi wa rangi kiungo wa Bolton
Fabrice Muamba baada ya kupoteza fahamu uwanjani katika mchezo dhidi ya Tottenham
Hotspur.
No comments:
Post a Comment