Didier Drogba katika style yake ya ushangiliaji |
Aliyekuwa
mshmabulizi wa Chelsea Didier Drogba amehamia klabu ya Shanghai Shenhua ya
China.
Kujiunga na
klabu hiyo kunamsogeza karibu na jamaa yake wa karibu toka Chelsea wakati huo Nicolas
Anelka.
Didier Drogba akiwa na mkewe Lalla |
Drogba mwenye umri wa miaka 34 amesema kabla ya kuamua kuhamia China alifikiria kwa makini maamuzi yake.
"Nilitilia maanani mialiko chungu nzima niliopata katika kipindi cha wiki chache zilizopita , lakini nafikiri kwa wakati huu kuhamia timu ya Shanghai Shenhua ulikuwa uamuzi mzuri"
Drogba akiwa katika moja ya maonyesho ya mavazi |
Nyota huyo raia wa Ivory Coast atakumbukwa kwa bao alilofungia Chalsea walipocheza na Bayern Munich ya Ujerumani.Bao hilo liliifanya Chalsea ijiandikie historia ya kushinda kombe la Klabu bingwa bara Ulaya.
Drogba alijiunga na Chalsea mwaka wa 2004 kutoka Olympic Marseille ya Ufaransa kwa pauni million 24. Alikuwa baadhi ya wachezaji wa kwanza kusajiliwa na Meneja Jose Mourinho alipojiunga na Chalsea.
Akiwa Chalsea kwa kipindi cha miaka minane, Drgoba aliisaidia klabu hiyo kushinda kombe la ligi kuu ya Uingereza mara tatu na kombe la FA mara nne.
Anaondoka Chalsea akiwa ameandikisha historia ya kuifungia timu hiyo jumla ya magoli 157 hivyo kuwa mchezaji nambari nne katika kwa ufungaji wa magoli katika historia ya Chalsea.
Kujiunga kwake na timu hiyo ya Shanghai Shenhua , Drogba anasema jukumu lake la kwanza ni kufanya soka ya China itambulike duniani.
No comments:
Post a Comment