KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Wednesday, June 20, 2012

EURO 2012 GOLI LA UTATA BLATTER ASEMA NENO - ENGLAND VS UKRAINE (READ DESCRIP...



Rais wa shirikisho la soka duniani Fifa Sepp Blatter amesema teknolojia ya “goal-line” ilikuwa muhimu baada ya baada ya kuzuka gumzo na malalamiko toka kwa mashabiki kwenda kwa waamuzi wa mchezo baina ya Uingereza na Ukraine wa Uefa Euro 2012 mchezo uliopigwa hapo jana.
 Marco Devic alidhani amepata goli la kusawazisha kwa waandaaji wenza goli ambalo endapo lingekubaliwa lingewapa nafasi ya kufuzu hatua ya robo fainali ya michuano hiyo lakini waamuzi toka nchini Hungary aliashiria mchezo kuendelea baada ya mpira huo kuondoshwa katika eneo la hatari na mlinzi John Terry.
 Kwa mujibu wa onyesho la marudio kupitia Television ilionekana wazi kuwa mpira huo ulivuka mstari wa goli na kocha wa Ukraine Oleg Blokhin na kikosi kizima cha timu hiyo walionekana kukasirika wakati Uingereza wakisema ilikuwa bahati kwao.
Tecknolojia ya “Goal-line” inatarajiwa kuidhinishwa na Bodi ya kimataifa ya chama cha soka (IFAB) ambayo inasimamia sheria za mchezo July 5.
Blatter kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter ameandika akisema kulihitajika tecknolojia ya goli katika mchezo wa jana pengine ingesaidia na kwamba sasa haitachukua muda na ni muhimu.
"After last night's match, GLT (goal line technology) is no longer an alternative but a necessity,"

No comments:

Post a Comment