Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi ya Yanga jaji John Mkwawa
Taarifa zilizo ifikia
Rockersports zinasema kuwa kikao cha kusikiliza mapingamizi kimefanyika salama
bila ya wapingaji kuwepo katika kikao hicho kilicho fanyika hii leo makao makuu
ya klabu ya Yanga.
Kikao hicho kilichokuwa
chini ya mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi ya Yanga Jaji John Mkwawa kilikuwa
kinasikiliza pingamizi dhidi ya wagombea watano wa nafasi mbalimbali za uongozi
akiwemo Yusufu Manji na Sarah Ramadhani wanaowania nafasi ya Mwenyekiti.
Wengine ni Yono Kevella, Clement Sanga na Ally Mayay
wanao wania nafasi ya makamu mwenyekiti.
Jaji Mkwawa hata hivyo
alitumia maelezo ya mapingamizi yaliyowasilishwa dhidi ya wagombea hao kuwahoji
wagombea juu ya hoja zilizomo ndani ya mapingamizi huku kila mmoja akitoa
utetezi wake na baadaye kujiridhisha na utetezi wao.
Kwasasa kinachosubiriwa
ni taarifa ya majumuisha ya kikao hicho ambayo kimsingi itatoa nafasi kwa
wanachama wa klabu hiyo kuelewa nini kilicho chomoza baada ya kikao hicho.
No comments:
Post a Comment