Konstantinos Chalkias mlinda mlango mstaafu wa Ugiriki |
Kichapo cha
Ugiriki cha mabao 4-2 toka kwa Ujerumani hatua ya robo fainali ya michuano ya UEFA
EURO 2012 kimepelekea wakongwe Konstantinos Chalkias na Nikos Liberopoulos kutangaza
kustaafu soka la kimataifa.
Mlinda mlango
wa PAOK Chalkias kwasasa ana um
ri wa miaka 38 amekuwa ndiye mchezaji mkubwa
kuliko wote wa michuano hii ya EURO 2012.
Amekaririwa Chalkias ambaye ameichezea timu ya
taifa ya Ugiriki jumla ya michezo 32 akisema amefurahia michuano hii na
kuongezea.
"huu
ulikuwa ni mwezi wa furaha sana katika maisha ya uchezaji wangu mpira. Sasa najikia
fahari ilikuwa ndoto yangu kumalizia soka yangu hapa".
"najikia
fahari na furaha kushiriki katika jitihada za kuifikisha Ugiriki katika robo
fainali"
Chalkias
alinza fainali hizi kama mlinda mlango namba moja lakini alishindwa kuendelea
kutokana na kupatwa majeraha katika mchezo wa pili dhidi ya Jamhuri ya Czech.
Mstaafu wa soka la kimataifa Ugiriki mkongwe Nikos Liberopoulos |
Kwa upande wake shambiliaji Liberopoulos ambaye kwasasa ana umri wa miaka 36 alianza kuitumikia timu ya taifa ya Uguriki mwaka 1996 amesema maamuzi ya kustaafu ni kama kuiacha familia yako.
Liberopoulos ambaye hakuwemo katika kikosi cha Ugiriki mwaka 2004 lakini miaka minne baadaye akafanikiwa kuwemo kikosini amesema alishawishika kuacha soka baada ya mchezo dhidi ya Ujerumani.
Aliingia uwanjani toka benchi katikati ya kipindi cha pili lakini akashindwa kuongeza goli loa 13 katika michuano ya kimataifa.
Amenukuliwa mchezaji huyo wa AEK Athens akisema
"nahisi kubariki kuufunga ukurasa huu katika timu ambayo kwangu mimi ni kama familia"
"ni heshima kubwa kwangu. Baada ya mchezo kwisha nilihisi kutokutaka kuondoka uwanjani "
Liberopoulos aliwahi kutangaza kuachana na soka la kimataifa 2009 kabla ya kocha wa wakati huo Fernando Santos kumshawishi kurejea uwanjani mwaka mmoja baadaye yaani 2010.
No comments:
Post a Comment