Kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza |
Timu ya
taifa ya Uingereza England itakuwa katika jaribio la kuhakikisha inafikia
katika hatua ya nusu fainali ya michuano mikubwa kwa mara ya kwanza ndani ya
kipindi cha miaka 16 jumapili wakati watakapo kuwa na kazi ya kuikabili Italia
katika moja ya michezo mikubwa na migumu ya Euro 2012.
Hali ya
kujiamini ndani ya kikosi cha vijana wa kocha Roy Hodgson inatiwa dosari na
rikodi mbaya ya Uingereza kutokufikia hatua ya timu nane za mwisho katika
michuano mbaya ikiondolewa mara tatu katika robo fainali ndani ya miaka 10
iliyopita.
Lakini baada
ya kushinda katika mchezo wa kundi D mbele ya Ufaransa na kuendeleza rekodi ya
kutokufungwa katika michezo mitano iliyopita Uingereza itakuwa ikielekea katika
mchezo wa kesho jumapili kule Kiev ikiwa
na hali ya kujiamini kuwa wataendelea kusalia katika michuano hiyo.
Kocha wa Uingereza Roy Hodgson |
Steven
Gerrard, Ashley Cole, Ashley Young, James Milner na Alex Oxlade-Chamberlain wote
wana kadi moja moja za njano kiasi huenda kama hawatajilinda vizuri wanaweza
kukosekana katika mchezo wa nusu fainali dhidi ya ama Ujerumani au Ugiriki
endapo wakifanikiwa kupenya katika mchezo wa kesho.
Hodgson hata
hivyo ana kazi ya kuwaeleza wachezaji wake kutokucheza hiyo kesho kwa yahadhari
ya kuogopa kusimamishwa kwa adhabu ya mchezo wa nusu fainali kwani inaweza
kuharibu uwezo wao katika mchezo huo.
Hodgson anatarajiwa
kuanziasha kikosi kilicho pata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ukraine jumanne na
sehemu ya ulinzi wa kati ikiongozwa na Milner ambaye atakuwa upande wa kulia na
mbele yake ni Theo Walcott.
Kwa upande
wake kocha Cesare Prandelli atalazimika kufanya mabadiliko katika ulinzi wa
kati kufuatia majeruha yanayomsibu kiungo wake hodari Giorgio Chiellini ambaye
nafasi yake itazibwa na Leonardo Bonucci.
No comments:
Post a Comment