KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Friday, June 22, 2012

USAJILI SIMBA:MLINZI WA DRC CONGO KUZIBA PENGO LA YONDANI

GLADYS BOKESE
 Katika kujaribu kuziba pengo la nafasi ya mlinzi wa kati ambayo imeachwa na mlinzi kitasa Kelvin Yondani aliyejiunga na klabu ya Yanga hivi karibuni , mabingwa klabu ya Simba inakamilisha usajili wa mlinzi wa timu ya taifa ya DRC Congo Gladys Bokese ambaye ni mchezaji huru.
Gladys Bokese ambaye alikuwa akiitumikia  kwa mara ya mwisho klabu ya
 Étoile Sportive du  Sahel ya Tunisia alitarajiwa kuwasili nchini Tanzania hii leo akitokea nchini Congo tayari kukamilisha taratibu za usajili.
Taarifa zilizoifikia Rockersports zimesema mchezaji huyo alikuwa apokelewe na makamu mwenyekiti wa Simba Geofrey Nyange Kaburu uwanja wa ndege wa kimataifa wa mwalimu Nyerere saa 10:00 jioni ya leo.
BOKESE AKIWA KATIKA MAJUKUMU YA KITAIFA
  Gladys Bokese alizaliwa September 9, 1981 jijini Kinshasa ambako aliaanza kucheza soka akiwa na klabu ya AS Bandal akicheza kama mshambuliaji.
Toka Bandal alijiunga na Daring Club Motema Pembe kifupi DC Motema Pembe akiwa na wachezaji kadhaa nyota kama Mbala Mbuta Biscotte na Ngasanya Ilongo.
Alianza kuichezea timu ya taifa ya Congo mwaka 2006 na kuwa ni miongoni mwa wachezaji waliounda kikosi kilichoshiriki fainali za mataifa ya Afrika mwaka huo.
Alipojiunga na timu ya taifa kocha wa timu ya taifa ya Congo Claude Le Roy alimbadilisha nafasi ya uchezaji na kumtumia kama mlinzi wa kati eneo ambalo amelimudu vema na mpaka sasa akiwa ni mlinzi wa kati tegemeo.
Taarifa za uhakika za mchezaji huyo kuja Tanzania zimethibitishwa na ndugu wa karibu wa mchezaji huyo ambaye amekuwa na mahusiano mazuri na Blogger hii.
BOKESE AKISHANGILIA GOLI

Viongozi wa Simba wamekuwa wagumu kuzungumzia juu ya hilo licha ya kuthibitisha kuwa mchezaji alikuwa akisubiriwa uwanja wa ndege na makamu mwenyekiti wa Kaburu.

No comments:

Post a Comment