Kamati ya uchaguzi ya Yanga ikiendelea na zoezi la usaili ndani ya makao makuu ya klabu hiyo (picha msaada Bin Zubeir) |
Hatimaye
zoezi la usaili kuelekea katika uchaguzi wa klabu ya Yanga limekamilika ambapo wagombea wote
waliopitishwa na kamati ya uchaguzi ya klabu hiyo wamepata nafasi ya kusailiwa
hii leo na kamati hiyo isipokuwa wagombea wawili tu Jamali kisongo na abdalaha sharia Ameir ambao wameshindwa kufika
katika zoezi hilo.
Akizungumza
na waandishi wa habari katika makao makuu ya klabu hiyo baada ya zoezi la
usaili katibu wa kamati ya uchaguzi Fransis Kaswahili amesema baada ya zoezi
hilo kinachofuata sasa ni wanachama kupata nafasi ya kuweka pingamizi juu ya
wagombea waliosailiwa na kupitishwa na kamati ya uchaguzi ya klabu hiyo ambapo
sasa mapingamizi yataelekezwa katika kamati ya uchaguzi ya shirikisho la
kandanda nchini TFF kuanzia june 24 mpaka
june 26.
Kswahili
ameongeza kuwa kamati ya uchaguzi ya TFF itakutana june 29 kupitia mapingamizi
hayo kabla ya kutangazwa kwa majina ya wagombea Julay mosi na kampeni kuanza
rasmi kwa wagombea waliopitishwa julai 3.
Aidha
amesema kampeni zitafanyika kwa wiki mbili mpaka julai 14 na uchaguzi
utafanyika julai 15.
Yusufu Manji akiwa na baadhi ya wanachama wa klabu ya Yanga kabla ya zoezi la usaili (picha kwa msaada wa Bin zubeir blog) |
Wagombea waliopitishwa katika zoezi la usaili ni Yusufu Manji , John Jambele , Edger Chibura na Sara Ramadhani ambao wanawania nafasi ya mwenyekiti.
Kwa upande wa nafasi ya mwenyekiti ni Ayoub Nyenzi, Yono Kevela na Clement Sanga.
Wanao wania ujumbe ni ni Lameck Nyambaya, Ramadhani Mzimba ‘Kampira’, Mohamed Mbaraka, Ramadhani Said, Edgar Fongo, Beda Simba, Ahmad Gao, Mussa Katabaro, George Manyama, Aaron Nyanda, Abdallah Bin Kleb, Omary Ndula, Shaaban Katwila, Jumanne Mohamed Mwammenywa, Abdallah Mbaraka, Peter Haule na Justin Baruti.
Kwa upande wake mgombea wa nafasi ya mwenyekiti mfanya biashara maarufu nchini Yusufu manji amewataka wanachama na wapenzi wa klabu hiyo kuwa watulivu kipindi hiki ambacho klabu hiyo bado iko katika mchakato wa uchaguzi lakini pia timu ya Yanga ikiwa katika maandalizi ya michuano ya Kagame.
amewataka pia wanachama wa Yanga watambue kuwa klabu ya Yanga kwasasa iko nyuma sana kimaendeleo na haina kocha na kwamba wanachama wanapaswa kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa amani ili viongozi watakao patikana waweze kuiletea yanga maendeleo.
Manji pia akatahadhari kama hali ya migogoro itaendelea ndani ya Yanga kila kukicha klabu hiyo haitakuwa na maendeleo daima
No comments:
Post a Comment