Release No. 102
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Juni
29, 2012
YANGA KUANZIA KWA ATLETICO
KOMBE LA KAGAME
Mabingwa watetezi wa Klabu
Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kombe la Kagame) wataanza kutetea ubingwa wao
Julai 14 mwaka huu dhidi ya Atletico ya Burundi kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam.
Katibu Mkuu wa Baraza la
Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), Nicholas Musonye
ametangaza ratiba ya michuano hiyo leo (Juni 29 mwaka huu) katika mkutano na
waandishi wa habari uliofanyika ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF).
Timu 11 zitashiriki katika
michuano hiyo itakayoanza Julai 14 hadi 28 mwaka huu ambapo kwa siku zitachezwa
mechi mbili (saa 8 mchana na saa 10 jioni) huku Tanzania Bara ikiwakilishwa na
Yanga, Simba na Azam. Mechi ya kwanza siku ya ufunguzi (saa 8 mchana) itakuwa
kati ya APR ya Rwanda na Wau Salaam ya Sudan Kusini.
Kundi A lina timu za Simba,
URA ya Uganda, Vita Club ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) na Ports ya
Djibouti. Azam, Mafunzo ya Zanzibar na Tusker ya Kenya ziko kundi B.
Yanga inaunda kundi C lenye
timu za APR ya Rwanda, Wau Salaam ya Sudan Kusini na Atletico ya Burundi.
Timu nane zitaingia robo
fainali itakayochezwa Julai 23 na 24 mwaka huu. Kundi A na C kila moja litatoa
timu tatu kwenda robo fainali wakati B litatoa timu mbili.
El Merreikh ya Sudan, Red Sea
ya Eritrea, Coffee ya Ethiopia na Elman ya Somalia hazitashiriki katika
mashindano ya mwaka huu ambayo yanafanyika Tanzania Bara kwa mwaka wa tatu
mfululizo kutokana na sababu mbalimbali.
Coffee haitashiriki kwa vile
ligi ya Ethiopia inaanza Julai 14 mwaka huu wakati El Merreikh wikiend ya Julai
13-15 mwaka huu itakuwa na mechi ya michuano ya Shirikisho la Mpira wa Miguu
Afrika (CAF).
Bingwa wa michuano hiyo
atapata dola 30,000, makamu bingwa dola 20,000 na mshindi wa tatu dola 10,000.
Michuano hiyo itaoneshwa moja kwa moja (live) na Televisheni ya
SuperSport.
KAGAME
CUP 2012 FIXTURE
Sat. 14th
July 1 APR vs WAU SALAAM Uwanja wa
Taifa 2pm
2 YANGA vs ATLETICO
Uwanja wa
Taifa 4pm
Sun. 15th
July 3 AZAM vs MAFUNZO
Chamazi
4pm
Mon. 16th
July 4 VITA CLUB vs PORTS
Uwanja wa Taifa
2pm
5 SIMBA vs URA
Uwanja wa
Taifa 4pm
Tue. 17th
July 6 ATLETICO vs APR
Uwanja wa Taifa
2pm
7 WAU SALAAM vs YANGA Uwanja
wa Taifa 4pm
Wed. 18th
July 8 VITA CLUB vs URA
Uwanja wa Taifa
2pm
9 PORTS vs SIMBA
Uwanja wa
Taifa 4pm
Thu. 19th
July 10 ATLETICO vs WAU SALAAM Uwanja wa
Taifa 2pm
11 MAFUNZO vs TUSKER
Uwanja wa Taifa
4pm
Fri. 20th
July 12 PORTS vs URA
Uwanja wa Taifa
2pm
13 YANGA vs APR Uwanja wa
Taifa 4pm
Sat. 21st
July 14 AZAM vs TUSKER
Uwanja wa Taifa
2pm
15 SIMBA vs VITA CLUB Uwanja wa
Taifa 4pm
Sun. 22nd
July REST DAY
QUARTER
FINALS
Mon. 23rd
July 16 B2 vs C2
17 A1 vs C3
Tue. 24th
July 18 C1 vs A2
19 B1
vs A3
Wed. 25th
July REST DAY
SEMI
FINALS
Thu. 26th
July 20 Winner 16 vs Winner 17
Thu. 26th
July 21 Winner 18 vs Winner 19
Fri. 27th
July REST DAY
FINALS
AND 3rd PLACE PLAY OFFS
Sat. 28th July
22 Loser 20 vs Loser 21
23 Winner 20 vs Winner 21
Boniface
Wambura
Ofisa
Habari
Shirikisho la
Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
No comments:
Post a Comment