Hali ya Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni
na Michezo Dokta FENELLA MUKANGARA aliyepata ajali leo asubuhi katika barabara
ya Nzega-Shinyanga inaendelea Vizuri.
Msaidizi
wa Waziri Ndugu JUMA MSADIKO ameiambia ROCKERSPORTS kwa njia ya simu kuwa taratibu
zinaendelea kufanywa ili kuangalia uwezekano wa kumpeleka Waziri huyo katika
hospitali ya Mkoa wa Dodoma kwa ajili ya matibabu zaidi.
Amepata
ajali ya gari katika Wilaya ya Nzega Mkoani Tabora akiwa njiani kwenda Mkoani
Mwanza kikazi.
Habari
kutoka Wilayani Nzega zinasema kwamba ajali hiyo imetokea wakati Waziri huyo
akiwa njiani akitokea Dodoma kwenda Mkoani Mwanza kuzindua Mashindano ya
Vishale.
Kulingana na Msaidizi huyo wa Waziri, gari limepinduka
mara Tatu wakati likilikwepa roli lilikokuwa mbele yao na Waziri huyo amepata
majeraha kadhaa katika mwili wake.
No comments:
Post a Comment