KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Friday, June 29, 2012

Fabregas:Spain itabidi kumdhibiti Pirlo ili kuwafunga Italy


Cesc Fabregas

Andrea Pirlo
kiungo wa kimataifa wa timu ya taifa ya Hispania Cesc Fabregas ametangaza kuwa kunahitajika hadhari kwa timu yake kama inataka kuifunga Italia katika mchezo wa fainali wa euro 2012 kumdhibiti Andrea Pirlo.
Kiungo huyo ambaye amekuwa akiicheza vizuri katika kikosi cha Azzurri alikuwa pia kwenye kiwango katika mchezo wa jana ambapo Italia ilichomoza na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Ujerumani.
Fabregas anaogopa uwezo wa kiungo huyo wa Juventus alioonyesha katika michuano hii ya EURO 2012 na kueleza kuwa alivutiwa na kiwango cha Mario Balotelli dhidi ya Ujerumani.
Ananukuliwa Fabregas amenukuliwa akisema
"tunalazimika kumdhibiti Pirlo".
"Balotelli ni mchezaji mzuri na alionyesha hilo jana. Alifunga mabao mawili dhidi ya Ujerumani kwenye nusu fainali Germany.
Del Bosque yuko tayari kukabili kingo cha Italia.
Kocha Del Bosque wa Hispania
Kocha wa timuya taifa ya Hispania ameanza kuonyesha wasiwasi juu ya uwezo wa La Roja timu ya taifa ya Italia kuelekea kwenye mchezo wa fainali ya jumapili ya Euro 2012 na kusema bado kuonyesha kile ambacho kipo katika uwezo wa kikosi licha ya kuendelea kutawala michezo mbalimbali.
Kocha wa Hispania Vicente del Bosque amesema kikosi chake kinapaswa kuwa sawasawa sehemuya kiungo katika mchezo wa jumapili wa fainali.
La Roja ilikuwa katika wakati mgumu jumatano usiku kiasi mikwaju ya penati kuamua matokeo ya mchezo baada ya sare ya bila kufungana dhidi ya majirani zao Ureno.

No comments:

Post a Comment