![]() |
Fabio Capello |
Chama cha
mpira cha Urussi kimethibitisha habari za kua aliyewahi kua Kocha wa klabu ya
Real Madrid na England Fabio Capello ndiye Kocha mpya wa Timu ya Taifa ya nchi
hiyo.
Punde baada
ya kutangazwa Capello mwenye umri wa miaka 66 amesema shabaha yake ni ufanisi
wa haraka. Ledngo langu ni kuiwezesha Urussi kufuzu kwa michuano ya Kombe la
Dunia nchini Brazil, alisema Capello.
Nilipomaliza
kazi ya England, nilikua na ghadhabu na nilitaka kuendelea kufanya kazi. Ukweli
ni kwamba nataka kutimiza malengo yenu Urussi na kufuzu kwa Kombe la Dunia
nchini Brazil.
Capello
alikuwa kwenye orodha ndefu iliyokuwa na majina ya magwiji kama Harry Redknapp,
ambaye chama cha mpira cha Urussi kilimtaka awe Kocha wake mpya.
Kocha huyo
aliacha sifa ya kiwango kikubwa cha ushindi kuliko waliomtangulia England
akishinda asili mia 67% ya mechi ingawa Timu yake ilipata shida kwenye
mashindano ya Kombe le Dunia nchini Afrika ya kusini mwaka 2010 ilipoondolewa
mapema na Ujerumani.
No comments:
Post a Comment