![]() |
Kikosi kamili cha timu ya Azam katika picha ya pamoja |
Baraza la
vyama vya soka Afrika mashariki na kati CECAFA limeipongeza klabu ya Azam kwa
kufanikiwa kushiriki kwa mara ya kwanza na hatimaye kutinga fainali ya michuano ya vilabu bingwa inayoendelea hivi sasa
jijini Dar es Salaam kwa mara ya kwanza
katika historia ya michuano hiyo.
Kauli hiyo
ya pongezi imetolewa na katibu mkuu wa baraza hilo Nikolaus Musonye hii leo
alipokuwa akiongea na waandishi wa habari katika ofisi za shirikisho la soka
hapa nchini TFF.
Pamoja na
pongezi hizo kwa Azam CECAFA pia imesema timu zote zilizofika fainali zimefika
hapo kihalali na kwamba hakuna timu iliyobebwa na kwamba kila timu Yanga ambao
ndio mabingwa watetezi na Azam zote zimefika hapo kwa uwezo wao.
Azam na
Yanga kesho zitakuwa zikiingia katika mchezo wa fainali ambao utaanza kupigwa
saa kumi kamili jioni huku mchezo wa kusaka mshindi wa tatu ukipangwa kuanza
saa saba kamili mchana.
CECAFA
imesema viingilio vya mchezo wa kesho vitabaki kama ilivyokuwa katika michezo
ya nusu fainali yaani sh. 5,000, sh.
7,000, sh. 15,000 na sh. 20,000.
CECAFA pia
imetoa pongezi kwa serikali kwa kuwapa huduma zote zinazostahili za uwanja
lakini pia pongezi nyingine zikienda kwa mashabiki ambao wameendelea
kushangilia timu za kwa ustaarabu na nidhamu kubwa.
No comments:
Post a Comment