Kundi
la kwanza la Cameroon likiongozwa na kiungo wa zamani wa Toulouse ya
Ufaransa ambaye sasa yuko Al Ahli ya Falme za Kiarabu (UAE), Achille
Emana na Meneja wa timu hiyo Rigobert Song litatua nchini kesho
(Februari 3 mwaka huu) saa 4.40 usiku kwa ndege ya KLM.
Wachezaji
wengine katika kundi hilo ni Vincent Aboubakary anayechezea timu ya
Valenciennes iliyoko Ligi Kuu ya Ufaransa, kipa Charles Itandje
anayedakia timu ya POAK FC ya Ugiriki, Kocha wa viungo Sylvain Monkam.
Mshambuliaji
wa Anzhi Makhachkala ya Urusi ambaye ndiye nahodha wa Cameroon, Samuel
Eto’o ataongoza kundi la pili litakalowasili nchini Februari 4 mwaka huu
(saa 3.45 asubuhi) kwa ndege ya Kenya Airways kupitia Nairobi, Kenya.
Wengine
katika ndege hiyo Herve Tchami wa Budapest Honved ya Hungary, beki
Nicolas Nkoulou wa Marseille ya Ufaransa, mshambualiji Jean Paul Yontcha
wa SC Olhanense ya Ureno na daktari wa timu Dk. Boubakary Sidik wakati
Kocha wa timu hiyo Jean Paul Akono na msaidizi wake Martin Ndtoungou
watawasili saa 4.40 asubuhi kwa ndege ya Kenya Airways akitokea Afrika
Kusini.
Februari
4 mwaka huu kuna kundi lingine litakaloingia saa 4.40 usiku kwa ndege
ya KLM ambalo lina beki Jean Kana Biyick wa Rennes ya Ufaransa,
mshambuliaji Fabrice Olinga wa Malaga FC ya Hispania, beki Allan Nyom wa
Udinese ya Italia ambaye yuko kwa mkopo Granada ya Hispania na beki wa
kushoto Henri Bedimo wa Montpellier ya Ufaransa.
Wachezaji
waliobaki wakiongozwa na kiungo wa Barcelona, Alexandre Song watawasili
Februari 5 mwaka huu kwa muda tofauti kwa ndege za KLM na Kenya
Airways.
No comments:
Post a Comment