TENGA AONGEZA WAWILI KAMATI YA NIDHAMU
Rais
wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodegar Tenga ameteua
wajumbe wawili kuingia kwenye Kamati ya Nidhamu ya TFF baada ya nafasi
mbili kuwa wazi kutokana na mmoja kuteuliwa kuongoza kamati nyingine ya
TFF na mwingine kufariki dunia.
Iddi
Mtiginjolla ambaye alikuwa mjumbe wa Kamati ya Nidhamu hivi karibuni
aliteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Rufani ya Uchaguzi ya TFF baada
ya Shirikisho kufanya mabadiliko ya katiba yaliyotokana na maagizo ya
Shirikisho la Kimataifa la Vyama vya Mpira wa Miguu (FIFA), wakati
mjumbe mwingine wa Kamati ya Nidhamu, Shaaban Semlangwa alifariki dunia
katikati ya mwaka uliopita.
Wajumbe
wapya walioteuliwa ni Jesse Mguto- alikuwa Hakimu Mkazi na kwa sasa ni
mwanasheria na Wakili wa Mahakama Kuu. Ana Digrii ya Sheria. Mwingine ni
Yohane Masala ambaye kwa sasa ni Mwanasheria Mwandamizi wa Serikali
(Principal State Attorney). Ana Digrii ya Kwanza na ya Pili ya Sheria na
Digrii ya Pili katika masuala ya Amani na Haki (MA in Peace and
Justice).
Rais
Tenga amesema ana imani na uwezo wa watu hao na kwamba watafanya kazi
yao kwa uadilifu ili Shirikisho liendelee kuboresha utawala bora.
No comments:
Post a Comment