Fransis kaswahili
Ikiwa
imesalia siku moja kabla ya uchaguzi mkuu mdogo wa kujaza nafasi za wajumbe wa
kamati ya utendaji ya Yanga kufanyika, kamati ya uchaguzi ya Yanga imesema mwanachama
yoyote atakaye elekea mahakamni kwa lengo la kujaribu kuzuuia uchaguzi huo
kufanyika atafutwa uanachama wake ndani ya klabu hiyo na kuhukumiwa kwa mujibu
wa kanuni za fifa .
kauli hiyo
imetolewa na katibu wa kamati ya uchaguzi ya Francis Kaswahili wakati akiongea
na waandishi wa habari makao makuu ya klabu hiyo kufuatia tishio la baadhi ya
wanachama la kutaka kuelekea mahakamani kupinga kile kinacho daiwa ni
kuenguliwa kwa baadhi ya wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya Yanga.
Hata hivyo
Kaswahili ameshindwa kutaja majina ya wanachama hao huku tayari tetesi
zikizagaa juu ya kuwepo kundi Fulani la wanachama waliojipanga kuelekea
mahakamni kuzuia uchaguzi kufanyika tarehe 15/07/2012 kama ilivyotangazwa na
kamati ya uchaguzi ya Yanga.
Lakini
wakati hayo yakiwa hivyo kamati hiyo imepokea malalamiko ya kuwepo kwa kampeni
chafu ambazo hata hivyo ameshindwa kuzithibitisha kuwa zimekuwa zikifanywa na
nani mbali ya kuonyesha kipeperushi ambacho kimeonyesha majina ya baadhi ya
wagombea na kikieleza kuwa hao ndio viongozi watakao iongoza Yanga.
Kaswahili
amesema endapo watabainika wanao fanya kampeni ya aina hiyo adhabu itatolewa.
kipeperushi
hicho kina majina ya wagombea na nafasi zao kama ifuatavyo
mwenyekiti –Yusufu
Manji
makamu
mwenyekiti- Clement Sanga
wajumbe –
Katabalo
-
Nyambaya
-
Manyama
-
Bin
Kleb
Aidha kuelekea
kwenye uchaguzi jumapili kamati hiyo ya uchaguzi ya Yanga imesema ifikapo kesho
kesho saa nane mchana ndio itakuwa mwisho wa kulipa ada kwa wanachama .
Siku ya
uchaguzi milango itafunguliwa saa tano zoezi la upigaji kura litaanza saa sita
na uhakiki mlangoni utasimamiwa na jeshi la polisi.
scout
watashughulikia masuala yote ya ndani kama kubeba mabox ya kura na marufuku
mgombea yoyote kusimama na kumpendekeza mgombea Fulani awe kiongozi.
No comments:
Post a Comment