Aliyekuwa
Rais wa shirikisho linalotawala mchezo wa soka duniani, FIFA , Joao Havelange (pichani juu)
pamoja na kiongozi wa soka wakati mmoja nchini Brazil Ricardo Teixeira
wanatuhumiwa kupokea mirungura ya mamilioni ya dola za kimarekani kama hongo
katika kupanga mwenyeji wa Kombe la Dunia, kwa mujibu wa tangazo la FIFA
lililochapishwa jumatano.
Hatimaye
shirikisho hilo limechapisha hati ya maelezo kamili kuwa Texeira alipokea
faranga za Uswizi milioni 12.74 sawa na dola za Marekani milioni 13 kwa kiwango
cha leo kuanzia mwaka 1992 hadi 1997 kama malipo kwa kampuni ya mauzo ya FIFA
ikiwa ni mshirika wa ISL. Kufilisika kwa kampuni hiyo yenye makao yake Uswizi
kulizusha upelelezi wa kihalifu na kufichua tabia mbovu iliyokuepo ya viongozi
kupokea mirungura ili kufanikisha mipango ya wanaohitaji.
Hati hio
yenye kurasa 41 ilionyesha kuwa Havelange alipokea malipo ya faranga za Uswizi
milioni 1.5 sawa na $milioni moja mnamo mwaka 1997, mwaka mmoja kabla ya
kumpisha Sepp Blatter kama Rais mpya.
Malipo
yanayotajwa kuwa yalipitia benki za raia hao wawili wa Brazil zilifikia kiwango
cha faranga milioni 22 za Uswizi kati ya mwaka 1992 na 2000.
Kiwango cha
mirungura inayohusiana na hati miliki ya kutangaza Kombe la Dunia pamoja na
haki ya kupitisha matangazo wakati wa Kombe la Dunia ilidhihirishwa katika
taarifa iliyotayarishwa na mwanasheria wa Wilaya ya Uswizi ya Zug
aliyewachunguza Havelange na Texeira kwa matumizi mabaya ya fedha au uongozi
usioambatana na misingi ya kazi.
Waraka huu
mwanzoni uliwekewa kizuizi usichapishwe tangu Juni mwaka 2010, baada ya
wanasheria, FIFA na watu wawili mashuhuri katika Soka duniani kuafikiana juu ya
kusimamisha upelelezi wa kihalifu.
FIFA,
Havelange na Teixeira walirejesha faranga milioni 5.5 million za Uswizi
(takriban dola $6.1 wakati huo) ili mwanasheria Thomas Hildbrand asimamishe
uchunguzi na majina yao yawe ni siri.
Teixeira,
ambaye alirejesha faranga milioni 2.5, alikanusha madai ya kuhusika kihalifu.
Havelange, aliyerudisha laki tano za Uswizi, hakutoa tamko lolote kuhusiana na
madai ya uhalifu, kwa mujibu wa taarifa hio.
No comments:
Post a Comment