Al Salaam
Wau klabu bingwa ya Saudan Kusini hii leo imenja tamu na chungu ya michuano ya Kagame
baada ya kuchapwa jumla ya mbao 7-0 na APR ya Rwanda mchezo wa kwanza na wa
ufunguzi wa michuano ulipigwa katika uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.
Huu ulikuwa
ni mchezo wa kwanza wa michuano ya mwaka huu lakini pia ni mchezo wa kwanza
klabu bingwa ya kusini kusini kushiriki tangu kujiunga na michuano hiyo nchi
ambayo ilipata uhuru wake wa kwanza jumatatu iliyopita.
Katika sehemu
ya shamra shamra ya uhuru wan chi hiyo kulikuwa na mchezo wa kwanza wa kirafiki
wa kimataifa ambapo 'Bright Star' ilikwenda sare ya bao 2-2
Group A: Simba (Tanzania), URA (Uganda), AS Vita Club (DR Congo), Ports
(Djibouti)
Group B: Azam (Tanzania), Mafunzo (Zanzibar), Tusker (Kenya)
Group C: Yanga (Tanzania), APR (Rwanda), Al Salaam Wau (South Sudan),
Atletico (Burundi)
Licha ya
kupata kichapo hicho kocha wa Al Salaam's Mel Yok Kuol alionekana mwenye furaha
na kiwango cha wachezaji wake.
APR ilipata
mabao yake matatu katika kipindi cha kwanza kupitia kwa Lionel St Preus, Jean
Baptist Mugireneza na mkongwe Olivier Karekezi.
St Preus akaandika
bao la pili kipindi cha pili huku Seleman Ndikumana akiandika bao linguine kabla
ya Barnabe Mubumbyi akiandika bao la saba.
Licha ya
kuwa wepesi wa kupoteza mpira Al Salaam walikuwa na nafasi za kutengeneza
nafasi za kufunga laikini ugeni katika michuano ilikuwa ni kikwazo kwa maana ya
kukosa uzoefu.
Nafasi nzuri
ilipotezwa na nahodha Khamis Leon dakika ya 60 ambapo mpira wake ulikwenda moja
kwa moja kwa mlinda mlango wa APR Jean Claude Ndoli.
Kocha wa Al
Salaam Sebit Bol Chol amekiri wachezaji wake kukosa uzoefu.
No comments:
Post a Comment