Timu ya
bandari ya Mombasa inatarajia kufanya ziara nchini Tanzania ambapo itakuwa na
michezo miwili ya kirafiki.
Timu hiyo
ambayo inashiriki ligi daraja la kwanza nchini Kenya hivi karibuni iliwasajili
wachezaji watatu toka nchini Tanzania akiwemo Mohamed Banka , Meshack Abel na
Thomas Morice.
Akiongea na
Rockersports toka Mombasa nchini Kenya kiungo Mohamed Banka amesema tayari
uongozi wa Bandari umethibitisha juu ya ujio wao hapa nchini na kwamba
wanatarajia kuwasili nchini jumanne tayari kwa mchezo wao wa kwanza dhidi ya Yanga
jumatano kabla ya mchezo wa pili dhidi ya Coast Union ya Tanga utakao fanyika
katika uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga.
Bandari
ambayo ili wahi kumsajili huko nyuma mlinda mlango Ivo Mapunda, kwasasa
inaongoza ligi daraja la kwanza nchini Kenya kwa idadi kubwa ya mabao ikiwa imeiacha timu inayo ifuata kwa tofauti
ya points 12.
Banka
amesema kwasasa wamekuwa kivutio kikubwa nchini Kenya kiasi mashabiki wa soka
na wapenzi wa Bandari wamekuwa wakifurika uwanjani kwenda kuangali huduma yao
ndani ya klabu hiyo ambayo kimsingi mashabiki wamekuwa wakiridhika.
Banka
amesema Meshack amekuwa lulu katika timu hiyo kama ilivyo kwa Thomas Morice
ambaye amekuwa akipachika mabao kila anapo pata nafasi ya kufanya.
No comments:
Post a Comment