Pascal Ochieng |
Klabu ya Simba
kukamilisha ITC za Kinje na Ochieng
Klabu ya
Simba imesema iko katika hatua nzuri ya kukamilisha suala la hati ya kimataifa
ya uhamisho ITC ya wachezaji wake wawili Salum Kinje na Pascal Ochieng.
Akiongea na
Rockersports afisa habari wa Simba Ezekiel Kamwaga amesema wana matumaini ya
kukamilisha suala hilo ndani ya masaa 48 yajayo na kwamba kwasasa kuna ujumbe
wa Simba jijini Nairobi nchini Kenya unafuatilia kazi hiyo.
Hivi karibuni shirikisho la soka nchini
lilitoa orodha ya wachezaji ambao wameombewa ITC na vilabu mbalimbali nchini
kutoka nje ya nchi ambapo kwa upande wa Yanga na tayari ITC zao zimepatikana ni
Nizar Khalfan kutoka Vancouver Whitecaps ya Canada, Didier Kavumbagu (Atletico
Olympic- Burundi) na Mbuyu Twite kutoka FC Lupopo ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya
Congo (DRC).
Kwa upande
wa Simba ni Musa Mude (Sofapaka, Kenya) na Daniel Akuffor (Stella Abidjan,
Ivory Coast) wakati Mtibwa Sugar ni Shabani Kisiga timu ya El Itihad ya Oman.
Waliopata ITC kwa upande wa Kagera Sugar ni
Wilfred Ojodale Ame na Benjamin Efe Ofuyah wote kutoka FC Abuja ya Nigeria.
Wengine ni Deangelis Silva kutoka New Road ya Nepal kwenda Coastal Union,
George Odhiambo kutoka Randers FC ya Denmark kwenda Mtibwa Sugar na Jerry Santo
kutoka Tusker, Kenya kwenda Coastal Union.
TFF ilisema
wachezaji ambao wameombewa usajili na ITC zao bado hazijapatikana ni Salum
Kinje na Pascal Ochieng wa Simba kutoka AFC Leopards.
TFF imetaka klabu
ambazo hazijakamilisha usajili na kupata ITC zina fursa ya kufanya hivyo hadi
Septemba 4 mwaka huu ambapo dirisha litafungwa.
No comments:
Post a Comment