Afellay kuondoka Barcelona kwa mkopo
Wakala wa Ibrahim
Afellay , Rob Jansen, ameweka wazi kuwa mchezaji huyo wa kimataifa wa uholanzi
yuko mbioni kuihama Barcelona kwa mkopo.
nyota huyo
wa zamani wa PSV anaonekana kama ni mtu asiye na umuhimu kwasasa katika kikosi
cha Barcelona kiasi hata kuachwa katika kikosi ambacho kiliifunga Osasuna kwa
mabao 2-1 mwishoni mwa juma.
Afellay yuko
mbioni kuondoka ili akatafute timu mbayo atapata nafasi ya kucheza katika
kikosi cha kwanza na mpango huo wa mkopo unaonekana kuwa ukingoni.
Jensen
amenukuliwa na Studio Voetbal
"ni
mchezaji mwenye kiwango cha mafanikio Barcelona, lakini kilicho mrudisha nyuma
ni majeraha. Itakuwa vema kujaribu kupata sehemu ambayo atacheza. Kwasasa tuko
katika mchakato kuangalia uwezekano,".
Afellay alijiunga
na Barcelona akitokea PSV mwezi January 2011, lakini majeraha yamemnyima fursa
ya kuonyesha uwezo msimu uliopita.
Mwamuzi anasema Coentrao alimuita mtoto wa
Malaya (son
of a w***e) ndiyo kisa cha kumpa
kadi nyekundu.
Mwamuzi Miguel
Angel Perez Lasa ameeleza juu ya maamuzi yake ya kumpa kadi nyekundu ya moja
kwa moja Fabio Coentrao katika mchezo ambao Real Madrid ilipoteza kwa kufungwa
mabao 2-1 mchezo wa ligi ya Hispania ‘La Liga’ dhidi ya Getafe hapo jana.
amenukuliwa Perez
Lasa kupitia taarifa yake ya baada ya mchezo ambayo imemnukuliwa na gazeti la
Marca akisema
"kunako
dakika ya 88 , mchezaji namba (5) Fabio Alexandre Da Silva Coentrao alitolewa
nje kutokana na sababu ifuatayo: alikabiliana na mimi wakati mchezo ukiwa
umesimama na kunitukana nilipokuwa nimesimama karibu yake na kuniita mtoto wa
malaya".
Kadi hiyo
haina madhara kwa mchezo wa pili wa marudiano wa Spanish Supercopa dhidi ya Barcelona,
isipokuwa ni kwa michezo ligi ya Hispania La Liga.
Madrid ilifungwa
mabao 3-2 katika mchezo wa kwanza Camp Nou wiki iliyopita ambapo mchezo wa
marudiano utapigwa Santiago Bernabeu jumatano ijayo.
Real Madrid wamnunua Modric toka Spurs
kwa euro
milioni €37
Luka Modric amefanikiwa
katika vipimo vya afya vya Real Madrid na rasmi amekamilisha uhamisho wake wa
ada ya euro milioni 37 kuondoka Tottenham, na ameingia mkataba wa miaka mitano
na Real Madrid.
Mabingwa hao
wa La Liga walikuwa wakifukuzia saini ya Modric katika kipindi chote cha majira
ya kiangazi ambapo hatimaye wamefanikiwa baada ya kukubaliana na Spurs.
Uhamisho
wake pia unajumuisha makubaliano ya mpango wa Urafiki "partnership
agreement" ambao kimsingi unatoa fursa kwa klabu hizo mbili kubadilishana wachezaji
na kocha ikiwa ni pamoja na kucheza michezo ya kirafiki.
Real Madrid imethibitisha
taarifa hiyo kupitia mtandao wa klabu hiyo ikisomeka
"Real
Madrid na Tottenham Hotspur wamekubaliana juu ya uhamisho wa Luka Modric, ambaye
atakuwepo katika klabu hii kwa miaka mitano . vilabu vyote viwili vimekubaliana
kujenga makubaliano ya ushirikiano."
Chicharito:Raha Manchester United kumsajili
Van Persie
Javier
Hernandez anaangalia mwelekeo mpya wa matumaini kwa kufanya kazi na
mshambuliaji Robin van Persie, huku akisisitiza kuwa ushindani katika sehemu
hiyo ya ushambuliaji utaisaidia Manchester United kufanya vema.
Mashetani
wekundu walilazimika kulipa pauni milioni £24 kumpata mduchi huyo ambaye aliifungia Arsenal jumla
ya mabao 30 msimu uliopita kabla ya kuonyesha mahaba ya kuelekea Emirates
Stadium.
Chacharito
amesema siku zote amekuwa akijifunza kutoka kwa Van Persie, ambaye amefunga
goli lake la kwanza akiwa na United katika mchezo dhidi ya Fulham jumamosi na
anaimani ataongeza nguvu ya kikosi.
Mshambuliaji
huyo mwenye umri wa miaka 24 alikuwa katika benchi akiaangalia bosi wake Sir
Alex Ferguson akiwaadhibu Cottagers kwa mabao 3-2, huku mshambuliaji wa
kimataifa wa Uholanzi na Shinji Kagawa wakisimamia sehemu ya ushambuliaji kwa
kutupia nyavuni kila mmoja.
Casillas akubali kukosolewa na Mourinho
Nahodha wa Real
Madrid Iker Casillas amesema yeye na wachezaji wenzake wanapaswa kuwajibika
kufuatia matokeo ya jana ambayo walipigwa kqwa mabao 2-1 na , lakini
amesisitiza Los Blancos can wanapaswa kujirekebisha baada ya kuanza vibaya
msimu.
Madrid walikuwa
wameanza vizuri baada ya bao la mapema la Gonzalo Higuain lakini wakapoteza
umakini katika kipindi cha pili na kujikuta wakipigwa mabao mawili ya Juan
Valera na Abdel Barrera.
Matokeo hayo
yameiacha Mdrid na point moja baada ya michezo miwili points tano nyuma ya
wapinzani wao wakubwa Barcelona.
Matokeo hayo
yamemfanya Jose Mourinho kuwa mwenye hasira na kuwanyooshea kidole wachezaji
akisema walikuwa katika kiwango cha kibaya isipokuwa hakuwa tayari kusema
lolote baada ya mchezo huo.
Casillas amekubali
ukosoaji huo, lakini kikubwa ni kuwa wameanza vibaya msimu kwa kuacha points
nyingi kama ilivyokuwa msimu uliopita dhidi ya Levante na Racing Santander kabla ya kurejea katika kasi ya ushindi.
Samuel Eto'o agoma kuichezea Cameroon
Samuel Eto'o
amekataa kuichezea timu ya taifa ya Cameroon kama mgomo dhidi ya kile
alichokielezea kama maandalizi mabaya yanayofanana na soka la ridhaa katika
timu ya taifa.
Mshambuliaji
huyo amejumuishwa katika kikosi kitakacho ikabili Cape Verde katika mchezo wa
kuwania kufuzu fainali ya mataifa ya Afrika baada ya kukamilisha kipindi cha adhabu
yake ya kusimama katika timu ya taifa miezi nane.
Lakini Eto'o
amesema kupitia barua yake kwenda shirikisho la soka la Cameroon kuwa yuko
tayari kurejea na kwamba huo si msimamo wake wa moja kwa moja
Eto'o, ambaye
ameicheza Cameroon jumla ya michezo 109 na kufunga jumla ya mabao 54 alifungiwa
kucheza soka la kimataifa na nchi yake kutokana na kufanya mgomo ulitopkana na
kutokulipwa kwa bonus za wachezaji baada ya michuano ya Morocco mwaka jana.
Shirikisho
la soka la Cameroon liliandika taarifa kwenda kwa Eto'o, mwanasheria wake na
klabu yake ya Anhzi Makhachkala kuwa adhabu ya mchezaji huyo imemalizika wiki
hii.
Kufuatia
taarifa hiyo kocha wa timu ya taifa Denis Lavagne alimjumuisha Eto'o katika kikosi
cha wachezaji 23 kwa ajili ya kuikabili face Cape Verde September 8 ukiwa ni
mchezo wa kwanza wa mzunguko wa mwisho kuwania kufuzu fainali za mataifa ya
Afrika 2013.
Mshambuliaji
huyo bado ameendelea kukuna kichwa kuhusiana na uongozi na usimamiaji mbaya wa
timu ya taifa, hasa timu ya taifa inapo safari mwendo mrefu kutumia
usafiri wa daraja la pili kwenye ndege.
No comments:
Post a Comment